Friday 12 May 2017

Wananchi Wilayani Siha watakiwa kuchukua tahadhari ya Mvua zinazoendelea kunyesha

Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Onesmo Buswelu amewataka wakazi na Wananchi wa Wilaya ya Siha kuchukua tahadhari ya kutosha wakati huu mvua zinapoendelea kwa wingi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo.

Hayo ameyasema wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo wa Serikali Wilayani Siha. Mhe Mkuu wa Wilaya ya Siha ameyasema hayo leo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha wakati alipohudhuria ufungaji wa mafunzo ya wataalam wa ugavi na manunuzi yaliyofanyika kimkoa katika Wilaya ya Siha.

Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kuwalinda watoto wao nyakati za kwenda shule na wakati wa kurudi nyumbani ili wasipatwe na janga la kuzolewa na maji ya Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Wilayani hapa.

No comments:

Post a Comment