Friday 2 October 2020

Halmashauri ya Siha yapongezwa na kuboresha stendi ya mabasi Sanya Juuu

Wakazi na Wananchi wa Wilaya ya Siha wameendelea kutoa pongezi kwa Halmashauri ya Siha kwa kuboresha kituo cha Mabasi Sanya Juu. Wanachi hao  hasa madereva na wamiliki wa magari ya abiria katika nyakati tofauti wameeleza kufurahishwa na miundombinu bora na imara iliyopo katika stendi hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha ndugu Ndaki Mhuli akiwa na viongozi wa dini hivi karibuni ambapo walitembelea stendi hiyo  alieleza kuwa  Halmashauri ya Siha imetumia zaidi ya shilingi Milioni 4 ya mapato ya ndani katika kuboresha miundombinu ya Stendi ya Sanya Juu na ile ya  KIA. 

 WANAFUNZI 2357 KUHITIMU ELIMU YA MSINGI SIHA 2020

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Siha ndugu Ndaki Mhuli amesema kuwa kati ya wanafunzi 2357 watakaomaliza darasa la saba tarehe 7-8/10/2020 wasichana ni 1230 na wavulana ni 1127 katika shule za msingi 59,Shule  za Serikali 53 na za mashirika na dini na binafsi ni shule 06

Maandalizi ya kufanyika kwa mtihani huo yameshakamilika na matarajio ya Halmashauri ni kuendelea kupata matokeo mazuri na kushika nafasi za juu kimkoa na Kitaifa alisema ndugu Ndaki Mhuli Mkurugenzi wa Halmashauri ya Siha

Friday 18 September 2020

 UWEZESHAJI WA WANANCHI KIUCHUMI-SIHA

Katika kipindi cha miaka 5  ya Serikali ya awamu ya tano Halmashauri  ya Siha imefanikiwa kutoa mikopo kwa vikundi 154 vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu vyenye wanufaika 2,629  ambapo  jumla ya  kiasi cha shilingi 439,399,843 zilitolewa na Halmashauri kutoka mapato ya ndani.

Fedha zilizotolewa ni sehemu ya  asilimia 10 ya  mapato ya ndani ya Halmashauri ya Siha kwa kuzingatia utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020

Tambua mafanikio ya Halmshauri ya Siha Sekta ya Maji yafikia asilimia 90

Katika kipindi cha miaka mitano 2015-2020 halmashauri ya Wilaya ya Siha imeendelea kuwa kinara katika usambazaji wa maji katika vijiji vyote 60,vitongoji 169 na Kata zote 17.

Hadi kufikia mwezi Septemba 2020 usambazaji wa maji Wilaya ya Siha umefikia  zaidi ya asilimia 90 ambapo  maji safi na salama yanapatikana wakati wote

Serikali ya awamu ya tano imetoa zaidi ya shilingi 3.7 bilioni  kwa ajili ya kugharamia  usambazaji na upanuzi wa miradi ya maji mikubwa na midogo Wilayani Siha.

Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya Uongozi dhabiti wa Serikali ya awamu ya tano ,halmashauri imejipanga kuhakikisha usambazaji wa maji unaongezeka hadi zaidi ya asilimia 95 ifikapo mwaka 2025.

Mafanikio ya Halmshauri ya Siha Sekta Barabara 2015-2020

Katika kipindi cha miaka mitano Halmasauri ya Siha imepokea kiasi cha shilingi 57.2 bilioni kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi na ukarabati a miundombinu ya barabara kwa kiwango  cha lami,changarawe na ukarabati wa barabara vijijini.

Fedha zilizotolewa na Serikali ya Tanzania zimesaidia ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa km 32.2 kutoka Sanya Juu hadi Elerai,ujenzi wa barabara za changarawe vijijini jumla ya km 199.2.

Barabara ya mwisho wa lami-Elerai

Pia Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Dkt. John Magufuli  imewezesha Madaraja muhimu kama vile  Kisube kirisha, Lawate loiwang, Muri - Nkwamariko na Mwaru.

Aidha,Serikali ya Tanzania kupitia wakala wa Barabara TARURA imefanikiwa kufanya ukarabati wa barabara zenye urefu wa km 236.81 na kuifanya halmashauri ya Siha kuwa miongoni mwa Halmashauri hapa nchini zenye barabara zinazopitika wakati wote wa mwaka.

Mafanikio haya yote yametokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Serikali na Wananchi wa Wilaya ya Siha pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya Wilaya.