Tambua
mafanikio ya Halmshauri ya Siha Sekta ya
Maji yafikia asilimia 90
Katika kipindi cha miaka mitano 2015-2020 halmashauri ya Wilaya
ya Siha imeendelea kuwa kinara katika usambazaji wa maji katika vijiji vyote
60,vitongoji 169 na Kata zote 17.
Hadi kufikia mwezi Septemba 2020 usambazaji wa maji Wilaya ya
Siha umefikia zaidi ya asilimia 90
ambapo maji safi na salama yanapatikana
wakati wote
Serikali ya awamu ya tano imetoa zaidi ya shilingi 3.7
bilioni kwa
ajili ya kugharamia usambazaji na
upanuzi wa miradi ya maji mikubwa na midogo Wilayani Siha.
Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya Uongozi
dhabiti wa Serikali ya awamu ya tano ,halmashauri imejipanga kuhakikisha
usambazaji wa maji unaongezeka hadi zaidi ya asilimia 95 ifikapo mwaka 2025.
No comments:
Post a Comment