Saturday 19 July 2014

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI DR TITUS KAMANI AKIZINDUA MASHINE YA UKATAJI WA CHAKULA CHA MIFUGO JUMATATU TAREHE 14.JULAI .2014 KATIKA KITUO CHA UTAFITI WEST KILIMANJARO-TALIRI



MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA SIHA MWENYE SHATI LA PINKI AKIMWONYESHA WAZIRI WA MIFUGO DR TITUS KAMANI ALIYEVAA KOTI LA KAKI MBELE BAADHI YA
MAENEO YA RANCHI YA WEST KILIMANJARO


WAZIRI KAMANI KUSHOTO AKIPOKEA MAELEKEZO YA RANCHI YA TAIFA WEST KILIMANJARO KUTOKA KWA MKUU WA WILAYA YA SIHA dR CHARLES MLINGWA ALIYEVAA SHATI JEUPE KATIKATI



BAADHI YA MAKUNDI MAKUBWA YA KONDOO WA KISASA WANAOPATIKANA KATIKA RANCHI YA TAIFA YA WEST KILIMANJARO ENEO LA NARCO NA TALIRI


MWAKILISHI WA TASAF KITAIFA MESE MANDAWA AKITOA MAELEZO MBALIMBALI YA MPANGO WA MRADI WA MFUKO WA JAMII TASAF KWA  WADAU MBALIMBALI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA TAREHE 17.07.2014. TASAF III INAMALENGO YA KUNUSURU KAYA MASKIN HAPA TANZANIA


WAHESHIMIWA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA WAKIPATA MAFUNZO YA MRADI WA TASAF III KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA HALMASHAURI HIYO TAREHE 17.JULAI.2014




DIWANI WA KATA YA LIVISHI WITSON NKINI AKICHANGIA MADA KATIKA MAFUNZO MAALUM YA TASAF III KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI YA SIHA TAREHE 17.07.2014.MPANGO HUU UNALENGA KUNUSURU KAYA MASKIN HAPA TANZANIA


WAKUU WA IDARA NA VITENGO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI MBALIMBALI SIKU YA UFUNGUZI WA MRADI WA TASAF III. ALIYEKAA KUSHOTO NI MESE MANDAWA MWAKILISHI WA TASAF TAIFA,ANAFUATIWA NA MKURUGENZI WA SIHA RASHID KITAMBULIO,KAIMU KATIBU MTENDAJI WILAYA YA SIHA BATILDA MHANDO NA MWISHO KULIA NI MAKAMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA SIHA DUNCAN URASSA


BAADHI YA WATAALAMU WA HALMASHAURI YA SIHA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA KATIKA UZINDUZI WA TASAF III SIKU YA ALHAMISI TAREHE 17.JULAI 2014

Tuesday 1 July 2014

HABARI KATIKA PICHA

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA SIHA RASHID KITAMBULIO ALITOA NASAHA ZAKE KWA WAKULIMA WA MAHINDI KIJIJI CHA WANRI HIVI KARIBUNI



WANACHAMA WA SACOSS YA WALIMU WA SIHA NA HAI WAKIFURAHIA MAFANIKIO YA CHAMA CHAO KATIKA UKUMBI WA RC SANYA JUU TAREHE 18.JUNI 2014



WANACHAMA WA SACOSS YA WALIMU WA SIHA NA HAI WAKISEREBUKA KATIKA MKUTANO WAO WA KAWAIDA KATIKA UKUMBI WA RC SANYA JUU HIVI KARIBUNI

Saturday 28 June 2014

 mwenyekiti wa kamati ya wa Elimu afya na Maji wilaya ya Siha Witson Nkini akitoa zawadi kwa Baadhi ya shule  za msingi zilifanya vizuri katika mashindano ya usafi Wilaya ya Siha


wanachama wa chama cha kuweka na kukopa kwa Walimu wa Siha na Hai wakiwa katika kikao chao cha mwaka katika ukumbi wa RC sanya juu hivi karibuni


wanachama hao wakicheza mziki kufurahia matunda ya chama chao ambacho kwa sasa kina zaidi ya wanachama 1700



ofisa wa elimu wilaya ya Siha Kushoto aliyevaa blauzi ya rangi ya maziwa Rozi Sandi akishiriki zoezi la kutoa zawadi kwa washindi wa mazingira katika shule za Msingi hivi karibuni

Saturday 7 June 2014

HABARI KATIKA PICHA

Mkuu wa Polisi wilaya ya Siha Afande Mwakyusa akikagua mzoga wa Tembo aliyekutwa amekufa mazingira ya kutatanisha kijiji cha karansi hivi karibuni.Wengine ni wananchi wa kijiji hicho walishuhudia tukio hilo




wanafunzi wa shule ya Sekondari Sanya Juu(Sanya Day) wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe wa siku
ya mazingira duniani iliyofanyika tarehe 05.06.2014 kwa zoezi la kupanda miti katika shule hiyo.zoezi hili liliwezeshwa na Jumuiya ya benki ya wananchi tanzania COBAT 


 

mwakilishi wa COBAT Bi Hellen Anchasein akipanda miti kati shule ya Sekondari Suumu katika maazimisho ya Siku ya Mazingira Duniani tarehe 05,06.2014


wanafunzi wa shule ya sekondari sanya Juu wakishiriki katika zoezi la uhifadhi wa mazingira katika kilele cha siku ya mazingira Duniani tarehe 05.06.2014
 zoezi la mazingira sanya Juu Sekondari





kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya siha Eliot Mwasbwite aliyevaa miwani kushoto alionesha masikitiko yake baada ya kufika eneo la tukio alipokufa tembo katika mazingira yasiyoeleweka

Saturday 17 May 2014

baadhi ya watumishi wa Wilaya ya siha waliofika katika moja ya vilele vya mlima kilimanjaro siku ya ijumaa tarehe 16.05.2014 katika kuitikia wito wa kuboresha utalii wa ndani ulitolewa na TANAPA


vijana wa wilaya ya Siha wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupata mafunzo ya utunzaji wa fedha yaliyotolewa na COBAT kwa ushirikaino na We Effect kutoka Sweden..mwenye nywele nyeupe wa Nne kutoka kulia ni Fuhanael Kihunrwa mmoja wa wawezeshaji katika mafunzo haya yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Amani sanya Juu

Monday 12 May 2014







jengo la kisasa la hospital mpya ya Halmashauri ya Wilaya ya Siha linalotegemewa kutumika katika siku za hivi karibuni katika kuimarisha huduma za afya kwa Wananchi wa Siha



wananchi wa kijiji cha Wiri kata ya Gararagua wakiitikia wito wa mkuu wa mkoa wa kilimanjaro wa Kuotesha miti katika maeneo mbalimbali ya kuzunguka eneo la ofisi ya kijiji cha Wiri





HILI NI LANNGO LA LONDOROSI GETI SEHEMU AMBAYO ITATUMIKA KUPANDA MLIMA  KILIMANJARO KATI YA TAREHE 15-18 2014 NA WATALII WA NDANI KUTOKA MKOA WA KILIMNAJARO (PICHA HAPA CHINI)






HALI ILVYOKUWA KATIKA UWANJA WA USHIRIKA MJINI MOSHI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI MEI MOSI 2014


Saturday 3 May 2014

ZOEZI LA UPANDAJI MITI KATIKA KATA YA GARARAGUA,KIJIJI CHA WIRI WILAYA YA SIHA

Mkuu wa Wilaya ya Siha Dr Charles Mlingwa akipokea taarifa fupi ya upandaji wa Miti katika Kata ya Gararagua iliyopo Wilayani Siha.zoezi hili limefanyika mwishoni mwa wiki
mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Wilaya ya siha ndugu Jonas  P.M akieleza jambo katika zoezi la upandaji miti kijiji cha Wiri mbele ya mkuu wa Wilaya ya Siha ambaye pichani hayupo

SHEREHE ZA MEI MOSI 2014 UWANJA WA USHIRIKA MJINI MOSHI

WAFANYAKAZI WAKIPONGEZANA KATIKA SHEREHE ZILIFANYIKA UWANJA WA USHIRIKA MJINI MOSHI.
BANGO LA WAFANYAKAZI KUTOKA HOSPITAL YA KIBONGOTO WILAYANI SIHA WAKIPITA MBELE YA MGENI RASMI NA UJUMBE WA MEI MOSI2014
SHAMBA LA MISITU WILAYANI SIHA LILILOPO WEST KILIMANJARO WAKIPITA MBELE YA MGENI RASMI MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO LEONIDAS GAMA WAKIWA NA GARI LENYE MICHE YA MITI KATIKA SHEREHE ZA MEI MOSI MWAKA 2014


bango la hospital ya taifa ya Kifua Kikuu iliyopo Wilayani Siha Wakitoa ujumbe wao kwa Wafanyakazi katika maadhimisho ya Mei Mosi 2014 katika Uwanja wa Ushirika Mjini Moshi

HABARI KATIKA PICHA


























mwenyekiti wa Halmashauri ya Siha Mheshimiwa Jonathan Nasari alisoma Taarifa yake mbele ya Baraza la Madiwani Siha tarehe 30.04.2014
BAADHI YA MADIWANI WA VITI MAALUMU WAKITETA JAMBO MARA BAADA YA KIKAO CHA  BARAZA LA MADIWANI TAREHE 30 04. 2014 KATIKA HALMASHAURI YA SIHA

Thursday 24 April 2014

WANAFUNZI 42 WAHITIMU KIDATO CHA SITA SANYA DAY


Wanafunzi 42 wamasomo ya sayansi na hisabati  wamehitimu kidato cha sita na kuwa wanafunzi wa kwanza waliosoma katika shule za serikali katika Wilaya ya Siha na kufikia hatua hiyo
Mahafali hayo yaliyofanyika katika shule ya Sekondari Sanya Juu kwa jina maarufu sanya Day yalihudhuriwa pia na wazazi wa wanafunzi hao 42 ndugu jamaa na marafiki wakiwemo wanafunzi wenzao
Mgeni rasmi katika maafali hayo yaliyofanyika leo tarehe 24.04.2014alikuwa ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Siha mheshimiwa Oscar Temi ambaye alifuatana na Wajumbe wengine na baadhi ya wazazi waliowasindikiza watoto wao
Katika mahafali hayo mwenyekiti huyo wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Siha aliwapongeza wanafunzi hao kwa hatua waliyofikia kimasomo na kuwashauri kuwa wasiishie hapo bali waendelee zaidi kimasomo
“Ndugu zangu nimesikia kilio chenu cha muda mrefu cha kukatikiwa na umeme mara kwa mara na hivyo kuwafanya msiweze kutimiza malengo yenu, mimi nitawasaidia kuweka Sola katika darasa moja ili mpake umeme wa kujisomea wakati wote hasa umeme wa kawaida unapoleta shida” mwenyekiti huyo alisema
Shule ya Sekondari Sanya Day ndiyo shule ya pekee  ya Serikali katika Wilaya ya siha yenye wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha Sita na ina jumla ya Wanafunzi 570 kwa sasa

Thursday 10 April 2014

HABARI KATIKA PICHA














zoezi la kupokea walimu wapya laendelea katika halmashauri ya Siha



kamanda wa vijana Wilaya ya Siha bwana Kelvin Maimu akila kiapo cha utii mbele ya mbunge wa siha Mh.Agrey Mwanri


mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama akitoa maelezo mafupi kwa wageni kutoka mtwara waliotembelea Wilaya ya siha tarehe 08/04/2014


mkuu wa Wilaya ya Siha Dr Charles Mlingwa akitoa maelezo mafupi kwa Wageni waliotembelea Wilaya ya Siha Kutoka Mkoa wa Mtwara hivi karibuni katika eneo la Darch Konna

wajumbe wa banki ya NMB HAI  pamoja na mkurugenzi wa halmashauri ya siha aliyevaa suruali nyeupe wakiwa  nje ya ofisi ya mkurugenzi wa Siha.wajumbe hawa walikuja kuhamasisha uanzishwaji wa banki hiyo wilaya ya siha tangu tarehe 25/03/2014




Wednesday 9 April 2014

MAHAKAMA KUU KANDA YA MOSHI YAWAACHIA HURU WASHTAKIWA 9 NA KUWATIA HATIANI 3 KATIKA KESI YA MAUAJI YA NMB MWANGA

Mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph Kanje ( aliyebeba mafaili),  Mshtakiwa namba moja, Samwel Gitau Saitoti (alifunika uso) na mwenzake  Mshtakiwa namba 2, Michael Kimani wakitoka nje ya mahakama kuu baada  ya mahakama hiyo kuwatia hatiani kwa kosa la kuua Askari polisi katika  tukio la uporaji wa benki ya NMB Mwanga
Washtakiwa namba 4 hadi 12, wakisaidiwa kupanda kwenye gari la Polisi baada ya mahakama kuu  kanda ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kuwaachia huru leo mchana katika kesi ya mauaji ya askari polisi yaliyotokea Julai 11 mwaka 2007.
Mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph Kanje ( aliyebeba mafaili),  Mshtakiwa namba moja, Samwel Gitau Saitoti (alifunika uso) na mwenzake  Mshtakiwa namba 2, Michael Kimani wakitoka nje ya mahakama kuu baada  ya mahakama hiyo kuwatia hatiani kwa kosa la kuua Askari polisi katika  tukio la uporaji wa benki ya NMB Mwanga.
Mshtakiwa namba 12, Salome Materu aliyekuwa Mhasibu wa Benki ya NMB  Mwanga akisaidiwa kupanda katika gari la polisi baada ya mahakama kuu  kanda ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kumuachia huru pamoja na wengine 8 katika kesi ya mauaji ya askari polisi yaliyotokea Julai 11 mwaka 2007.
Mshtakiwa namba 12, Salome Materu aliyekuwa Mhasibu wa Benki ya NMB  Mwanga akisaidiwa kupanda katika gari la polisi baada ya mahakama kuu  kanda ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kumuachia huru pamoja na wengine 8 katika kesi ya mauaji ya askari polisi yaliyotokea Julai 11 mwaka 2007..(picha zote  na Fadhili Athumani)
Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
MAHAKAMA kuu kanda ya Moshi, imewaachia huru washtakiwa 9 na kuwatia  hatiani wengine 3 wakiwemo Wakenya wawili na Mtanzania mmoja kwa kosa la kumuua askari Polisi E6829 Michael Milanzi, aliyeuawa katika tukio  la Ujambazi lilitokea Julai 11mwaka 2007 kwenye Benki ya NMB tawi laMwanga.

Akisoma uamuzi mdogo wa mahakama hiyo, Jaji mfawidhi Kasusulo Sambo alisema kwa mujibu wa sheria wa sheria 293 ya muendelezo wa ushahidi  wa makosa ya jinai, kifungu kidogo cha 1, sura ya 20 kamailivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, mahakama imeridhia kuwa Jamhuri  ilishindwa kabisa kujenga kesi dhidi ya watuhumiwa 9, Raia wa Tanzania, na hivyo inawaachia huru.

Jaji Sambo alisema katika uamuzi huo Mahakama vilevile ikiongozwa na sheria hiyo kifungu kidogo cha 2, sura ya 20 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002, imeona kwamba upande wa Jamhuri ilifanikiwa kujenga Kesi dhidi ya mshtakiwa namba 1, Samwel Gitau, Mshtakiwa namba mbili Michael Kimani, wote raia wa Kenya na mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph Kanje, Raia wa Tanzania.

 "Mahakama ilitafakari ushahidi wote wa Jamhuri, na kufikia maamuzi kwamba mashahidi wote 18 waliofika mbele ya mahakama hii, walionesha ni jinsi gani Jamhuri ilivyoshindwa kujenga kesi dhidi ya washtakiwanamba 4,5,6,7,8,9,10,11, na 12.

"Aidha Mahakama hii tukufu imeridhishwa kwamba Jamhuri kwa kuzingatia sheria ya muendelezo wa makosa ya jinai, kifungu kidogo cha pili, sura ya 20 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, ilifanikiwa kujenga kesi kwa kiwango kisicho mashaka dhidi ya washtakiwa namba 1,2 na 3,"alisema Jaji Sambo.

Katika uamuzi huo, Jaji Sambo aliongeza kuwa Mahakama inaamuru washtakiwa wote 4 hadi 12 walionekana kutokuwa na kesi ya kujibu dhidi ya tuhuma hiyo ya mauaji waachiwe huru maramoja isipokuwa kama wana kesi nyingine inayowakabili ambapo mtuhumiwa namba 10, ElizabethMsanze "Bella" ambaye anatuhuma za ujambazi alilazimika kuendelea kutumikia kifungo chake.

Washtakiwa walioachiwa huru ni mshtakiwa namba 4, Deodat Temu, mshtakiwa namba 5, Afande Nathaniel Wanyama, mshtakiwa namba 6, Emmanuel Mziray, mshtakiwa namba 7, Florian Kimati "Babylon", mshtakiwa namba 8 Devotha Msanze.

Wengine ni mshtakiwa namba 9, Juliana Msanze, Mshtakiwa namba 10 Elizabeth Msanze, mshtakiwa namba 11, Ntibasalila Msanze na mshtakiwa namba 12, Salome Materu ambaye alikuwa ni Mhasibu wa Benki hiyo wakati wa uvamizi.

Wakati huo huo upande wa utetezi unaomtetea mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph, unaowakilishwa na wakili wa kujitegemea, Prof. Jonas Itemba, umetoa ombi la kuwasilisha mashahidi wawili mahakamani hapo kwa ajili ya kutoa ushahidi wa utetezi kwa mteja wake.

Mashahidi hao ni Josephine Kalisti, ambaye ni mke wa Mshtakiwa huyo, raia wa Tanzania anayetuhumiwa kushiriki na kufadhili tukio la ujambazi lililopelekea mauaji, na mwengine ni Dafrosa Joseph.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa tena Aprili 10 mwaka huu, baada ya Mahakama kuridhia ombi la Washtakiwa namba 1 na 2 ambao hawana mashahidi, ya kutaka kuruhusiwa kuwasilisha mahakamani, maelezo ya Shahidi namba moja aliyoandika kwa mkono wake ambaye ni meneja wa Benki hiyo wakati huo, Robert Marandu.

Sunday 6 April 2014

habari katika picha


CCBRT WATOA HUDUMA ZAO KWA WALEMAVU SIHA



Shirika lisilo la kiserikali (CCBRT) tawi la Moshi leo limetoa huduma zake katika halmashauri ya wilaya ya siha katika Jengo jipya la Hospital ya Wilaya ya Siha lililopo karibu na mji mdogo wa sanya Juu
Shirika hilo lenye makao yake makuu Dar es salaam na lina tawi lake kubwa katika mji wa Moshi eneo la kaloleni Pasua leo limetoa huduma mbalimbali za kuwachunguza na kuwapatia matibabu na hasa ushauri kwa walezi wa walemavu ambao leo walifurika kwa wingi katika jingo hilo jipya la Hospital ya wilaya ya Siha

 Mkurugenzi wa CCBRT tawi la Moshi alisema kuwa baadhi ya huduma ambazo zinatolewa na shirika hilo kwa  watoto wenye umri chini ya miaka 18 na wanawake  ni pamoja na watoto  wenye matatizo ya Mpasuko wa mdomo(cleft Lip),Kuvuja mkojo kwa wanawake baada ya kujifungua(VVF),miguu iliyopinda kwenye nyayo 

Ruth Mlay mkurugenzi wa CCBRT-Moshi aliongeza kuwa mbali na huduma hizo pia wanatoa huduma kwa watoto wenye mtindio wa ubongo(cerebral Palsy),watoto wenye uvimbe Mgongoni(spina Bifida) na pia watoto wenye kichwa kikubwa (Hydrochephalus)
Akiongea katika shughuli hiyo  Daktari Mkuu wa Wilaya ya Siha Dr Best Magoma alisema kuwa jambo la kwanza walilolifanya ni kuwagundua walemavu wote katika Wilaya ya siha na maeneo wanayotoka. Alisema kuwa anawashukuru Wananchi wote wa Siha kwa kuitikia wito na kutoa ushirikiano wa kutosha hadi zoezi hili zimefankiwa kwa kiasi kikubwa

Pia Dr Best magoma aliwashukuru viongozi wa taasisi mbalimbali hasa taasisi za dini ambazo alisema zimetoa ushirikiano mkubwa sana wa kuhamasisha jamii hasa za vijijini kwa ajili ya kufanikisha kazi hii kubwa na yenye manufaa kwa jamii. Alisema kuwa Wilaya ya Siha hadi sasa inajumla ya walemavu mbalimbali wapatao 552 wenye ulemavu wa aina mbalimbali

Mkuu huyo wa Idara ya afya katika Wilaya ya Siha aliongeza kuwa walemavu wanayo haki ya kuishi na kujitegemea iwapo jamii itawajea uwezo badala ya kuwafungia ndani na kuwaona kama ni mkosi katika familia. Aliomba jamii kubadilika sasa na kuondokana na dhana potofu ya kuwatenga walemavu katika shughuli za kijamii

Afisa ustawi wa jamii ndugu Peter Msaka akiongea katika zoezi hilo alisema kuwa bado elimu zaidi inahitajika kwa jamii ili kuweza kuondokana na mila zisizo na maana za kuwatenga na kuwadharau walemavu katika jamii. Alitoa wito kwa jamii kuwa walemavu wasifichwe majumbani na badala yake  wapelekwe hospitalini mapema ili wapate matibabu