Thursday 22 September 2022

WATENDAJI WA VIJIJI SIHA WATAKIWA KUSIMAMIA VEMA UKUSANYAJI WA MAPATO YA HALMASHAURI


 

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro Upendo Mangali amewaagiza Watendaji wa Vijiji vyote 60 katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha kubuni vyanzo vipya vya mapato na kusimamia vema ukusanyaji wa mapato katika maeneo ya Vijiji husika.Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 22.9.2022 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha alipokuwa na kikao kazi na watendaji wote wa Vijiji 60 vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha ambapo amewataka kusimamia kwa ukaribu ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri katika vyanzo vilivyomo maeneo yao"Napenda kuwakumbusha watumishi wenzangu kuwa ninyi ndio wakurugenzi katika vijiji vyenu na ndio maofisa masuhuli katika maeneo yenu ya Vijiji hivyo ni budi mhakikishe kuwa mnakusanya mapato ya Halmashauri kwa ukamilifu ili yasaidie shughuli za maendeleo  na uboreshaji wa utoaji wa huduma katika Halmashauri yetu" alisema Mangali Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Siha.Lengo la kikao kazi kilichoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Siha  kwa Watendaji wa Vijiji ni pamoja na kuwakumbusha wajibu mbalimbali pamoja na kupatiwa  mafunzo Watendaji wa Vijiji kuhusu mfumo wa ulipaji wa fedha za Serikali kwa ngazi ya Vijiji