OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA
SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA
TAARIFA
YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI MKUTANO
WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI KATIKA KIPINDI CHA ROBO YA PILI (OKTOBA
-DESEMBA,2016).
v Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Siha,
v Mwakilishi Ofisi ya RAS-Mkoa wa
Kilimanjaro,
v Mh. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Siha,
v Mh. Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya
Siha,
v Waheshimiwa Madiwani,
v Mkurugenzi Halmashauri ya Siha,
v Viongozi wa Dini,
v Wageni Waalikwa,
v Ndugu Wataalamu,
v Waandishi wa Habari,
v Wananchi wa Wilaya ya Siha,
v Mabibi na Mabwana,
Wasalaam Alekumu,Tumsifu Yesu Kristo,Bwana
Yesu asifiwe
Wah. Madiwani , na Ndugu
Wananchi;
Naomba
tusimame kwa dk moja ili kuwakumbuka wale wote waliopoteza maisha katika
kipindi cha mwisho wa mwaka 2016 na hasa
mwenzetu Mheshimiwa Anna A Masaki diwani
wa viti maalum (W) alifariki mapema mwaka huu 2017
Habarini
za mwaka mpya 2017, ni matumaini yangu kuwa mmevuka mwaka salama na wote
mnaendelea na majukumu yenu ya
kuwatumikia wananchi kama kawaida.
(1)UTUNZAJI
WA CHAKULA
Waheshimiwa Madiwani na ndugu Wananchi.
Napenda
kuwaomba na kuwakumbusha tena Wananchi wa Halmashauri ya Siha kuhakikisha kuwa
tunakuwa na tabia ya kutunza chakula kilichopo kwani hali ya hewa kama mnavyoiona
kuwa siyo nzuri sana hasa baada ya mvua
ya vuli kukosekana. Mimi kama mwenyekiti wa Halmashauri ya Siha napenda kutoa
rai kwa Waheshimiwa Madiwani na Viongozi wengine katika ngazi za Kata na Vijiji
tushirikiane kwa pamoja kuwaelimisha wananchi kuhusu elimu ya utunzaji wa
chakula hasa katika ngazi ya Kaya na Vijiji. Pia nawaomba viongozi wa Madhehebu
ya Dini tushirikiane kwa pamoja katika kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu
wa utunzaji na uhifadhi wa chakula .
Kipekee namshukuru Mkuu wetu wa Wilaya ya Siha kwa kuweka agizo la kuzuia matumizi
ya mahindi katika kutengenezea pombe za kienyeji hasa Dadii(nzuga) kama sehemu
ya kunusuru matumizi ya nafaka yasiyo ya
lazima.
(2)UKUSANYAJI WA MAPATO
Waheshimiwa Madiwani,
Pamoja
na Halmashauri yetu kukabiliwa na tatizo ya vyanzo vichache na vya kudumu vya
mapato yake ya ndani, Halmashauri imeendelea kukusanya mapato yake ya ndani kwa
kutumia Vijiji vilivyopo katika maeneo
yenye vyanzo vya mapato na kwa kutumia
mashine za kieletroniki kukusanya mapato hayo kama ilivyoagizo la Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Hata hivyo Halmashauri ya Siha bado inakabiliwa
na changamoto kubwa ya ukosefu wa vyanzo vya uhakika na vya kudumu vya mapato hali ambayo inatufanya sisi sote kama
viongozi kuendelea kubuni vyanzo mbadala vya kuongeza mapato ya ndani ya
Halmashauri yetu.
(3) UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Waheshimiwa Madiwani,ndg Wananchi na Wataalam.
Ndugu
zangu hali ya ukame mnayoiona katika Wilaya yetu imetokana na shughuli za kibinadamu zilizosababisha
uharibifu mkubwa wa mazingira. Ili kunusuru hali hii isiendelee katika maeneo
yetu ya Wilaya ya Siha, naomba kutoa mapendekezo ya kila kaya kuotesha angalau
miti 5 kila mwaka na kama inawezekana tuweke kwenye sheria ndogo za Halmashauri
ambazo zitamtaka kila mwenye eneo la ardhi kuotesha miti ya kutosha kulingana
na ukubwa wa eneo lake. Kwa hili naomba kumwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Siha kuhakikisha kuwa Watendaji wa Kata na Vijiji katika
Halmashauri ya Siha kupitia vikao vya
Vijiji na Vitongoji wanawaelimisha wananchi kuhusu upandaji wa miti katika
maeneo yao. Pia wenye mashamba makubwa tutafanya utaratibu wa kuwaomba waotesha
miti angalau 500 kila mwaka ili kunusuru Wilaya ya Siha kugeuka kuwa jangwa.
Aidha,
najua adui mkubwa wa miti ni mifugo,naomba wote kwa pamoja tusaidiane kulinda
mifugo yetu ili isiharibu miti
tunayopanda kila mwaka.
(4)
MIFUGO KUTOKA NJE YA WILAYA
Waheshimiwa Madiwani,Ndugu Wananchi;
Naomba kutoa agizo kwa Viongozi wa Vijiji na
Kata hasa watendaji wa Vijiji kuhakikisha kuwa hakuna mifugo inayoingia ndani
ya vijiji na kata zetu kutoka Wilaya au mikoa jirani. Kimsingi mifugo hii inasababisha kuongezeka kwa
uharibifu wa mazingira Wilayani Siha na kusababisha kuongezeka kwa magonjwa ya
mifugo kwa mifugo yetu,mfano mzuri ni
ugonjwa hatari wa kimeta ambao kimsingi umetoka nje ya Wilaya yetu.naomba
viongozi wenzangu tusaidiane kulisimamia hili na pale inapopatikana mifugo
kutoka nje ya maeneo yetu basi hatua za kisheria zichukuliwe hasa za kutoza
faini stahili kulingana na sheria zilizopo ili kuongeza mapato ya Halmashauri. Ofisi
yangu inamwomba Mkuu wa Wilaya ya Siha kutusaidia jambo hili kwani wakati
mwingine litahitaji nguvu za dola katika kulitekeleza ipasavyo.
(5) UTUNZAJI WA BARABARA
Waheshimiwa Madiwani,Ndugu Wananchi;
Naomba tena kuwakumbusha wananchi wa Halmashauri ya Siha kuhakikisha kuwa kila
mmoja anashiriki kikamilifu katika kuzitunza
barabara zilizojengwa na Serikali katika Kata na Vijiji vyetu. Serikali inatoa
pesa nyingi kutengeneza barabara hizo ambazo zimeanza kuharibiwa na baadhi ya
watu kwa kuzikata kwa kupitisha mifereji au mabomba bila kibali cha Ofisi ya Mkurugenzi
Mtendaji. Naomba Mkurugenzi uwaagize watendaji wako wa Kata na Vijiji kwa
kushirikiana na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji kulisimamia agizo hili kwa ukaribu zaidi. Naomba kutoa agizo kuwa
kuanzia sasa ni marufuku kwa mtu yeyote kukata barabara bila kibali cha Mkurugenzi
Mtendaji na yeyote atakayekiuka hilo
achukuliwe hatua ili iwe fundisho kwa wenzake.
(6)UWAJIBIKAJI KAZINI
Waheshimiwa Madiwani,Ndugu Wananchi;
Napenda
kuwakumbusha tena Watumishi wa Serikali waliopo Wilaya ya Siha kuwa Serikali ya
awamu ya tano imeshasema kuwa haitawavumilia watumishi wazembe na wabadhirifu kazini.
Naomba kila mtumishi atimize wajibu wake kwa mujibu wa taaluma aliyosomea na
kwa kufuata sheria na taratibu za utumishi wa Umma.
Aidha
,naomba kuwakumbusha tena wazazi/walezi kuwa shule za msingi na sekondari
zimeshafunguliwa tangu mwezi wa
Januari,2017 na wajibu wao ni kuhakikisha
kuwa watoto wote wanakwenda shuleni na ni jukumu lao kuwawezesha watoto wao kupata chakula mashuleni. Naomba viongozi wote
tushirikiane kuwaelimishe wazazi/walezi
ili kutimiza majukumu ya kuwapatia mahitaji muhimu watoto wao hasa mlo wa
mchana.Elimu ni ufunguo wa maisha
kila mtu atimize wajibu wake.
Waheshimiwa Madiwani na ndg Wananchi;
Kabla
ya kufika mwisho wa Taarifa yangu, napenda
kuwashukuru tena Wananchi wa Wilaya ya
Siha na Waheshimiwa Madiwani kwa
ushirikiano wenu wa dhati mnaoendelea
kunipatia kwa ajili ya kutekeleza majukumu yangu ya Kila siku. Naomba kuchukua
fursa hii kuwahimiza wananchi wa Siha kujiandaa vema na msimu mkubwa wa mvua za
masika ambao tumezoea unaanza mwezi
Machi kila mwaka. Naomba wote kwa umoja wetu tufanye kazi kwa bidii kwa
maendeleo ya Familia zetu , Wilaya ya Siha na Taifa kwa ujumla wake.
Mwisho
,nichukue fursa hii kwa niaba ya baraza la Madiwani, kuwashukuru tena kwa
usikivu wenu mkubwa mlionesha tangu mwanzo wa taarifa yangu, naomba usikivu na
utulivu huu uendelee hadi mwisho wa mkutano wetu na hatimaye tumalize na
kuagana kwa upendo na furaha. Aidha,Napenda kuishukuru tena Ofisi ya Mkuu wa
Wilaya ya Siha kwa ushirikiano mzuri hasa wa kuhamasisha shughuli za maendeleo
katika Wilaya yetu
Asanteni sana kwa kunisikiliza
Imetolewa na:
Frank K. Tarimo
Mwenyekiti
wa Halmashauri (W)
SIHA
Tarehe 24.2.2017