Friday 2 November 2018

SERIKALI KUMALIZA KERO YA MAJI MUNGE


Serikali kuwapatia Maji Wananchi wa  Munge

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa fedha  zaidi ya shilingi  milioni 638 (638,000,000/-) kwa ajili ya kuondoa kero ya maji kwa wananchi wa kijiji cha Munge kata ya Donyomuruak Wilayani Siha.

Hayo yamesemwa leo tarehe 01/11/2018 na mkuu wa Wilaya ya Siha mhe. Onesmo  Buswelu  alipokuwa akimtambulisha kwa wananchi wa kijiji cha Munge  mkandarasi  atakayefanya kazi hiyo  kuanzia mwezi Novemba 2018 hadi Augusti 2019.
 Mkuu wa Wilaya ya Siha mhe. Onesmo Buswelu (katikati) akikagua miundombinu ya maji kijiji cha Munge
 Wananchi wa kijiji cha Munge wakimsiliza mkandarasi aliyepewa kazi na Serikali ya kupeleka  na kujenga mradi mkubwa wa maji  wenye thamani ya shilingi milioni 638
Matarajio ya mradi kukamilika ni mwezi Agosti,2019

Mkuu wa Wilaya ya Siha aliwaeleza wananchi kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi shupavu wa mhe. Rais John Pombe Magufuli imedhamiria kuondoa kero zote zinazoikabili jamii ikiwemo kero ya maji.

Hata hivyo mkuu wa Wilaya ya Siha alitoa wito kwa wananchi wa kijiji cha Munge na wale wa vijiji jirani kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa mkandarasi aliyepewa kazi hiyo ili kufanikisha dhamira ya Serikali ya kuwaletea maendeleo.

Awali akimkaribisha mkuu wa Wilaya ya Siha mhandisi wa maji Halmashauri ya Wilaya ya Siha Joyce Bahati kwa niaba ya mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha alieleza kuwa, mradi utakapokamilika utawanufaisha kaya zaidi ya 200 katika kijiji cha Munge kwa kuwapatia maji safi na salama.

Mhandisi huyo Alieleza kuwa,  mradi huo unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 10 kuanzia mwezi Novemba,2018, na jumla ya vilula 6 (vituo vya maji) vitajengwa katika maeneo mbalimbali ya kijiji cha Munge ili kusogeza  huduma ya maji karibu na wananchi.

Halmashauri ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro ni miongoni mwa Halmashauri zilizopata mafanikio makubwa katikaaidi sekta ya maji ambapo hadi mwezi Oktoba 2018,usambazaji na upatikanaji wa maji umefikia zaidi asilimia 85.


SERIKALI YATOA MIL 638 MRADI WA MAJI KIJIJI CHA MUNGE

 wananchi wa kijiji cha Munge wakimsikiliza mkuu wa Wilaya ya Siha alipofika kumtambulisha mkandarasi wa mradi wa maji kijiji hapo tarehe 1/11/2018
 baadhi ya wananchi wa kijiji cha Munge wakitoa shukurani kwa serikali ya Tanzania kwa kuwapatia fedha shilingi milioni 638 mradi wa maji


 wazee pia walikuwepo katika mapokezi ya mkandarasi kijiji cha Munge tarehe 1/11/2018
 Mkuu wa Wilaya ya Siha mhe. Onesmo Buswelu (katikati) akikagua miundombinu ya maji katika kijiji cha Munge

 Mhandisi wa maji halmashauri ya Wilaya ya Siha Joyce Bahati (kulia) akimueleza mkuu wa Wilaya eneo mradi utakapoanza kuchukua maji na kuyasambaza kijiji cha Munge kata ya Donyomuruak


Thursday 1 November 2018

WATAKAOWAPA MIMBA WANAFUNZI KUKIONA:DC SIHA


Mkuu wa Wilaya ya Siha mhe. Onesmo Buswelu ametoa onyo kali Wilayani Siha kwa watu wote wanaokatisha masomo wanafunzi wa kike kwa kuwasababishia mimba.

Hayo ameyasema katika kijiji cha Munge kata ya Donyomuruak tarehe 1/11/2018 alipokuwa akiongea na wananchi katika mkutano wa kijiji hicho uliotishwa kwa lengo la kumtambulisha mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi mradi mkubwa wa   maji.

Alieleza kuwa pamoja na kumtambulisha mkandarasi leo kwa wananchi napenda kutoa onyo kali kwa watu watakaothubutu kukatisha masomo  watoto wa kike kwa kuwasababishia mimba .

“Napenda kuwaeleza kuwa kwa hili siwezi kuwa na uvumilivu lazima nitahakikisha kuwa watu wote watakaowapa mimba wanafunzi wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao” alisema Buswelu.

Mkuu huyo wa Wilaya alitoa wito kwa wananchi na wakazi wa Wilaya ya Siha kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola pamoja na viongozi mbalimbali katika jamii ili kufanikisha zoezi la kuwatafuta na kuwakamata kwa haraka watu watakaodiriki kuwapa mimba wanafunzi.


Friday 12 October 2018

UJENZI WA BARABARA LAMI SANYA JUU-ELERAI

Wajumbe wa kamati ya siasa mkoa wa Kilimanjaro pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Siha na uongozi wa Chama cha Mapinduzi Siha wakikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya lami Sanya Juu hadi Elerai km 32.2










kazi ya ujenzi ikiendelea katika eneo la Dartch Kona karibu na Makao makuu ya Halmashauri ya Siha 



Mhe. Godwin Mollel Mbunge wa Jimbo la Siha akishiriki katika ukaguzi wa barabara hiyo eneo la Kata ya Ngarenairobi


wajumbe wa kamati ya Siasa ya mkoa wa Kilimanjaro na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Siha wakishiriki katika kukagua kazi ya ujenzi wa barabara hiyo eneo la Ngarenairobi


Mbunge wa jimbo la Siha mhe.Godwin Mollel (kulia) akikagua ujenzi huo eneo la Ngarenairobi West Kilimanjaro




Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa KILIMANJARO mhe BOY SAFI akitoa maelekezo ya juu ya ujenzi wa barabara hiyo  akiwa katika ofisi za mkandarasi GEO ENGENEERING CHINA  

Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Onesmo Buswelu (aliyevaa kofia) akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro kabla ya kuanza ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya lami km 32.2 Sanya Juu hadi Elerai 



Mhe Onesmo Buswelu(katikati aliyevaa kofia)  Mkuu wa Wilaya ya Siha akitoa maelezo kwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro kuhusu maendeleo ya ujenzi wa barabara ya lami Siha 

muonekano wa barabara inayojengwa eneo la Dartch kona karibu na makao makuu ya Halmashauri ya Siha



Tuesday 9 October 2018

HABARI ZA MATUKIO KATIKA PICHA

VIJANA WA CHIPUKIZI WILAYA YA SIHA WAKITOA SALAMU ZA UTII KATIKA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU SIHA TAREHE 29.09.2018

KARIBU SIHA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU TANZANIA NDG CHARLES FRANCIS KABEHO

MKUU WA WILAYA YA SIHA MHE ONESMO BUSWELU(KULIA) AKIPONGEZANA NA MKUU WA WILAYA YA HAI MARA BAADA YA MAKABIDHIANO YA MWENGE WA UHURU ,TUKIO LIMEFANYIKA KATIKA KIJIJI CHA LAWATE TAREHE 29.09.2018




MOJA YA TAARIFA ZA MIRADI YA MAENDELEO ALIYOKABIDHIWA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA NDG CHARLES FRANCIS KABEHO

VIJIJI VYOTE WILAYANI SIHA VYAPATIWA UMEME


ASILIMIA 100 VIJIJI WILAYANI   SIHA VINA UMEME
Wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro imefanikiwa kuvipatia vijiji vyake vyote 60 nishati ya umeme (ambayo ni sawa na asilimia 100) na hivyo kuongeza kasi ya wananchi kujiendeleza kiuchumi katika sekta mbalimbali.
Hayo yametolewa   na ndg Ismael Salum Meneja wa Shirika la Umeme Wilaya ya Siha tarehe 08/09/2018 katika kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya ya Siha, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha.

Kikao hicho chini ya Mwenyekiti Mhe. Onesmo Buswelu Mkuu wa Wilaya ya Siha walitoa pongezi nyingi kwa uongozi wa shirika hilo Wilaya ya Siha kwa huduma bora wanazoendelea kuzitoa kwa wananchi.

Meneja wa shirika la umeme Wilaya ya Siha alieleza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa maeneo yote katika Wilaya ya Siha yanakuwa na huduma ya umeme ili kuwezesha mpango wa Serikali ya Viwanda.

Wilaya ya Siha imefanikiwa kusambaza umeme kwa vijiji 60 kati ya 60 vilivyopo na hadi mwezi septemba, 2018 vitongoji 126 kati ya 169 vimepatiwa  huduma ya umeme.



AJIRA MPYA KADA YA AFYA HIZI HAPA


PATA NAFASI ZA KAZI AJIRA KADA YA AFYA TUMIA LINK :http://www.tamisemi.go.tz/announcement/ajira-mpya-kwa-kada-ya-afya-awamu-ya-pili

MAPOKEZI YA MWENGE SIHA TAREHE 29.09.2018

DC SIHA MHE.ONESMO BUSWELU AKIMPOKEA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA NDG CHARLES KABEHO



MBUNGE WA JIMBO LA SIHA MHE.DKT.GODWIN MOLLEL AKITOA SHUKRANI KWA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE ALIPOKUWA WILAYA YA SIHA 29.09.2018



MASISTA WA ST.HILDEGARD WAKIPOKEA MWENGE WA UHURU ULIPOTEMBELEA ZAHANATI YA ST.HILDEGARD KILICHOPO KIJIJI CHA NDINYIKA


MKURUGENZI MTENDAJI H.W SIHA VALERIAN JUWAL AKIPOKEA MWENGE WA UHURU ULIPOWASILI WILAYA YA SIHA TAREHE 29.09.2018



MKUU WA WILAYA YA SIHA MHE.ONESMO BUSWELU AKIMKABIDHI MWENGE WA UHURU MKUU WA WILAYA YA ROMBO