Mkuu wa Wilaya ya Siha mhe.
Onesmo Buswelu ametoa onyo kali Wilayani
Siha kwa watu wote wanaokatisha masomo wanafunzi wa kike kwa kuwasababishia
mimba.
Hayo ameyasema katika
kijiji cha Munge kata ya Donyomuruak tarehe 1/11/2018 alipokuwa akiongea na wananchi katika mkutano wa kijiji hicho
uliotishwa kwa lengo la kumtambulisha mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi mradi
mkubwa wa maji.
Alieleza kuwa pamoja na
kumtambulisha mkandarasi leo kwa wananchi napenda kutoa onyo kali kwa watu
watakaothubutu kukatisha masomo watoto
wa kike kwa kuwasababishia mimba .
“Napenda kuwaeleza kuwa kwa
hili siwezi kuwa na uvumilivu lazima nitahakikisha kuwa watu wote watakaowapa
mimba wanafunzi wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria ili hatua
stahiki zichukuliwe dhidi yao” alisema Buswelu.
Mkuu huyo wa Wilaya alitoa
wito kwa wananchi na wakazi wa Wilaya ya Siha kutoa ushirikiano kwa vyombo vya
dola pamoja na viongozi mbalimbali katika jamii ili kufanikisha zoezi la
kuwatafuta na kuwakamata kwa haraka watu watakaodiriki kuwapa mimba wanafunzi.
No comments:
Post a Comment