Serikali
kuwapatia Maji Wananchi wa Munge
Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania imetoa fedha zaidi
ya shilingi milioni 638 (638,000,000/-)
kwa ajili ya kuondoa kero ya maji kwa wananchi wa kijiji cha Munge kata ya
Donyomuruak Wilayani Siha.
Hayo yamesemwa leo tarehe
01/11/2018 na mkuu wa Wilaya ya Siha mhe. Onesmo Buswelu
alipokuwa akimtambulisha kwa wananchi wa kijiji cha Munge mkandarasi
atakayefanya kazi hiyo kuanzia
mwezi Novemba 2018 hadi Augusti 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Siha mhe. Onesmo Buswelu (katikati) akikagua miundombinu ya maji kijiji cha Munge
Wananchi wa kijiji cha Munge wakimsiliza mkandarasi aliyepewa kazi na Serikali ya kupeleka na kujenga mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 638
Matarajio ya mradi kukamilika ni mwezi Agosti,2019
Mkuu wa Wilaya ya Siha
aliwaeleza wananchi kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi shupavu wa
mhe. Rais John Pombe Magufuli imedhamiria kuondoa kero zote zinazoikabili jamii
ikiwemo kero ya maji.
Hata hivyo mkuu wa Wilaya
ya Siha alitoa wito kwa wananchi wa kijiji cha Munge na wale wa vijiji jirani
kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa mkandarasi aliyepewa kazi hiyo ili
kufanikisha dhamira ya Serikali ya kuwaletea maendeleo.
Awali akimkaribisha mkuu wa
Wilaya ya Siha mhandisi wa maji Halmashauri ya Wilaya ya Siha Joyce Bahati kwa niaba ya mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Siha alieleza kuwa, mradi utakapokamilika
utawanufaisha kaya zaidi ya 200 katika kijiji cha Munge kwa kuwapatia maji safi
na salama.
Mhandisi huyo Alieleza kuwa, mradi huo unatarajiwa kukamilika baada ya miezi
10 kuanzia mwezi Novemba,2018, na jumla ya vilula 6 (vituo vya maji) vitajengwa
katika maeneo mbalimbali ya kijiji cha Munge ili kusogeza huduma ya maji karibu na wananchi.
Halmashauri ya Wilaya ya
Siha mkoani Kilimanjaro ni miongoni mwa Halmashauri zilizopata mafanikio
makubwa katikaaidi sekta ya maji ambapo hadi mwezi Oktoba 2018,usambazaji na
upatikanaji wa maji umefikia zaidi asilimia 85.
No comments:
Post a Comment