Thursday 24 April 2014

WANAFUNZI 42 WAHITIMU KIDATO CHA SITA SANYA DAY


Wanafunzi 42 wamasomo ya sayansi na hisabati  wamehitimu kidato cha sita na kuwa wanafunzi wa kwanza waliosoma katika shule za serikali katika Wilaya ya Siha na kufikia hatua hiyo
Mahafali hayo yaliyofanyika katika shule ya Sekondari Sanya Juu kwa jina maarufu sanya Day yalihudhuriwa pia na wazazi wa wanafunzi hao 42 ndugu jamaa na marafiki wakiwemo wanafunzi wenzao
Mgeni rasmi katika maafali hayo yaliyofanyika leo tarehe 24.04.2014alikuwa ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Siha mheshimiwa Oscar Temi ambaye alifuatana na Wajumbe wengine na baadhi ya wazazi waliowasindikiza watoto wao
Katika mahafali hayo mwenyekiti huyo wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Siha aliwapongeza wanafunzi hao kwa hatua waliyofikia kimasomo na kuwashauri kuwa wasiishie hapo bali waendelee zaidi kimasomo
“Ndugu zangu nimesikia kilio chenu cha muda mrefu cha kukatikiwa na umeme mara kwa mara na hivyo kuwafanya msiweze kutimiza malengo yenu, mimi nitawasaidia kuweka Sola katika darasa moja ili mpake umeme wa kujisomea wakati wote hasa umeme wa kawaida unapoleta shida” mwenyekiti huyo alisema
Shule ya Sekondari Sanya Day ndiyo shule ya pekee  ya Serikali katika Wilaya ya siha yenye wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha Sita na ina jumla ya Wanafunzi 570 kwa sasa

Thursday 10 April 2014

HABARI KATIKA PICHA














zoezi la kupokea walimu wapya laendelea katika halmashauri ya Siha



kamanda wa vijana Wilaya ya Siha bwana Kelvin Maimu akila kiapo cha utii mbele ya mbunge wa siha Mh.Agrey Mwanri


mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama akitoa maelezo mafupi kwa wageni kutoka mtwara waliotembelea Wilaya ya siha tarehe 08/04/2014


mkuu wa Wilaya ya Siha Dr Charles Mlingwa akitoa maelezo mafupi kwa Wageni waliotembelea Wilaya ya Siha Kutoka Mkoa wa Mtwara hivi karibuni katika eneo la Darch Konna

wajumbe wa banki ya NMB HAI  pamoja na mkurugenzi wa halmashauri ya siha aliyevaa suruali nyeupe wakiwa  nje ya ofisi ya mkurugenzi wa Siha.wajumbe hawa walikuja kuhamasisha uanzishwaji wa banki hiyo wilaya ya siha tangu tarehe 25/03/2014




Wednesday 9 April 2014

MAHAKAMA KUU KANDA YA MOSHI YAWAACHIA HURU WASHTAKIWA 9 NA KUWATIA HATIANI 3 KATIKA KESI YA MAUAJI YA NMB MWANGA

Mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph Kanje ( aliyebeba mafaili),  Mshtakiwa namba moja, Samwel Gitau Saitoti (alifunika uso) na mwenzake  Mshtakiwa namba 2, Michael Kimani wakitoka nje ya mahakama kuu baada  ya mahakama hiyo kuwatia hatiani kwa kosa la kuua Askari polisi katika  tukio la uporaji wa benki ya NMB Mwanga
Washtakiwa namba 4 hadi 12, wakisaidiwa kupanda kwenye gari la Polisi baada ya mahakama kuu  kanda ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kuwaachia huru leo mchana katika kesi ya mauaji ya askari polisi yaliyotokea Julai 11 mwaka 2007.
Mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph Kanje ( aliyebeba mafaili),  Mshtakiwa namba moja, Samwel Gitau Saitoti (alifunika uso) na mwenzake  Mshtakiwa namba 2, Michael Kimani wakitoka nje ya mahakama kuu baada  ya mahakama hiyo kuwatia hatiani kwa kosa la kuua Askari polisi katika  tukio la uporaji wa benki ya NMB Mwanga.
Mshtakiwa namba 12, Salome Materu aliyekuwa Mhasibu wa Benki ya NMB  Mwanga akisaidiwa kupanda katika gari la polisi baada ya mahakama kuu  kanda ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kumuachia huru pamoja na wengine 8 katika kesi ya mauaji ya askari polisi yaliyotokea Julai 11 mwaka 2007.
Mshtakiwa namba 12, Salome Materu aliyekuwa Mhasibu wa Benki ya NMB  Mwanga akisaidiwa kupanda katika gari la polisi baada ya mahakama kuu  kanda ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kumuachia huru pamoja na wengine 8 katika kesi ya mauaji ya askari polisi yaliyotokea Julai 11 mwaka 2007..(picha zote  na Fadhili Athumani)
Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
MAHAKAMA kuu kanda ya Moshi, imewaachia huru washtakiwa 9 na kuwatia  hatiani wengine 3 wakiwemo Wakenya wawili na Mtanzania mmoja kwa kosa la kumuua askari Polisi E6829 Michael Milanzi, aliyeuawa katika tukio  la Ujambazi lilitokea Julai 11mwaka 2007 kwenye Benki ya NMB tawi laMwanga.

Akisoma uamuzi mdogo wa mahakama hiyo, Jaji mfawidhi Kasusulo Sambo alisema kwa mujibu wa sheria wa sheria 293 ya muendelezo wa ushahidi  wa makosa ya jinai, kifungu kidogo cha 1, sura ya 20 kamailivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, mahakama imeridhia kuwa Jamhuri  ilishindwa kabisa kujenga kesi dhidi ya watuhumiwa 9, Raia wa Tanzania, na hivyo inawaachia huru.

Jaji Sambo alisema katika uamuzi huo Mahakama vilevile ikiongozwa na sheria hiyo kifungu kidogo cha 2, sura ya 20 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002, imeona kwamba upande wa Jamhuri ilifanikiwa kujenga Kesi dhidi ya mshtakiwa namba 1, Samwel Gitau, Mshtakiwa namba mbili Michael Kimani, wote raia wa Kenya na mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph Kanje, Raia wa Tanzania.

 "Mahakama ilitafakari ushahidi wote wa Jamhuri, na kufikia maamuzi kwamba mashahidi wote 18 waliofika mbele ya mahakama hii, walionesha ni jinsi gani Jamhuri ilivyoshindwa kujenga kesi dhidi ya washtakiwanamba 4,5,6,7,8,9,10,11, na 12.

"Aidha Mahakama hii tukufu imeridhishwa kwamba Jamhuri kwa kuzingatia sheria ya muendelezo wa makosa ya jinai, kifungu kidogo cha pili, sura ya 20 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, ilifanikiwa kujenga kesi kwa kiwango kisicho mashaka dhidi ya washtakiwa namba 1,2 na 3,"alisema Jaji Sambo.

Katika uamuzi huo, Jaji Sambo aliongeza kuwa Mahakama inaamuru washtakiwa wote 4 hadi 12 walionekana kutokuwa na kesi ya kujibu dhidi ya tuhuma hiyo ya mauaji waachiwe huru maramoja isipokuwa kama wana kesi nyingine inayowakabili ambapo mtuhumiwa namba 10, ElizabethMsanze "Bella" ambaye anatuhuma za ujambazi alilazimika kuendelea kutumikia kifungo chake.

Washtakiwa walioachiwa huru ni mshtakiwa namba 4, Deodat Temu, mshtakiwa namba 5, Afande Nathaniel Wanyama, mshtakiwa namba 6, Emmanuel Mziray, mshtakiwa namba 7, Florian Kimati "Babylon", mshtakiwa namba 8 Devotha Msanze.

Wengine ni mshtakiwa namba 9, Juliana Msanze, Mshtakiwa namba 10 Elizabeth Msanze, mshtakiwa namba 11, Ntibasalila Msanze na mshtakiwa namba 12, Salome Materu ambaye alikuwa ni Mhasibu wa Benki hiyo wakati wa uvamizi.

Wakati huo huo upande wa utetezi unaomtetea mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph, unaowakilishwa na wakili wa kujitegemea, Prof. Jonas Itemba, umetoa ombi la kuwasilisha mashahidi wawili mahakamani hapo kwa ajili ya kutoa ushahidi wa utetezi kwa mteja wake.

Mashahidi hao ni Josephine Kalisti, ambaye ni mke wa Mshtakiwa huyo, raia wa Tanzania anayetuhumiwa kushiriki na kufadhili tukio la ujambazi lililopelekea mauaji, na mwengine ni Dafrosa Joseph.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa tena Aprili 10 mwaka huu, baada ya Mahakama kuridhia ombi la Washtakiwa namba 1 na 2 ambao hawana mashahidi, ya kutaka kuruhusiwa kuwasilisha mahakamani, maelezo ya Shahidi namba moja aliyoandika kwa mkono wake ambaye ni meneja wa Benki hiyo wakati huo, Robert Marandu.

Sunday 6 April 2014

habari katika picha


CCBRT WATOA HUDUMA ZAO KWA WALEMAVU SIHA



Shirika lisilo la kiserikali (CCBRT) tawi la Moshi leo limetoa huduma zake katika halmashauri ya wilaya ya siha katika Jengo jipya la Hospital ya Wilaya ya Siha lililopo karibu na mji mdogo wa sanya Juu
Shirika hilo lenye makao yake makuu Dar es salaam na lina tawi lake kubwa katika mji wa Moshi eneo la kaloleni Pasua leo limetoa huduma mbalimbali za kuwachunguza na kuwapatia matibabu na hasa ushauri kwa walezi wa walemavu ambao leo walifurika kwa wingi katika jingo hilo jipya la Hospital ya wilaya ya Siha

 Mkurugenzi wa CCBRT tawi la Moshi alisema kuwa baadhi ya huduma ambazo zinatolewa na shirika hilo kwa  watoto wenye umri chini ya miaka 18 na wanawake  ni pamoja na watoto  wenye matatizo ya Mpasuko wa mdomo(cleft Lip),Kuvuja mkojo kwa wanawake baada ya kujifungua(VVF),miguu iliyopinda kwenye nyayo 

Ruth Mlay mkurugenzi wa CCBRT-Moshi aliongeza kuwa mbali na huduma hizo pia wanatoa huduma kwa watoto wenye mtindio wa ubongo(cerebral Palsy),watoto wenye uvimbe Mgongoni(spina Bifida) na pia watoto wenye kichwa kikubwa (Hydrochephalus)
Akiongea katika shughuli hiyo  Daktari Mkuu wa Wilaya ya Siha Dr Best Magoma alisema kuwa jambo la kwanza walilolifanya ni kuwagundua walemavu wote katika Wilaya ya siha na maeneo wanayotoka. Alisema kuwa anawashukuru Wananchi wote wa Siha kwa kuitikia wito na kutoa ushirikiano wa kutosha hadi zoezi hili zimefankiwa kwa kiasi kikubwa

Pia Dr Best magoma aliwashukuru viongozi wa taasisi mbalimbali hasa taasisi za dini ambazo alisema zimetoa ushirikiano mkubwa sana wa kuhamasisha jamii hasa za vijijini kwa ajili ya kufanikisha kazi hii kubwa na yenye manufaa kwa jamii. Alisema kuwa Wilaya ya Siha hadi sasa inajumla ya walemavu mbalimbali wapatao 552 wenye ulemavu wa aina mbalimbali

Mkuu huyo wa Idara ya afya katika Wilaya ya Siha aliongeza kuwa walemavu wanayo haki ya kuishi na kujitegemea iwapo jamii itawajea uwezo badala ya kuwafungia ndani na kuwaona kama ni mkosi katika familia. Aliomba jamii kubadilika sasa na kuondokana na dhana potofu ya kuwatenga walemavu katika shughuli za kijamii

Afisa ustawi wa jamii ndugu Peter Msaka akiongea katika zoezi hilo alisema kuwa bado elimu zaidi inahitajika kwa jamii ili kuweza kuondokana na mila zisizo na maana za kuwatenga na kuwadharau walemavu katika jamii. Alitoa wito kwa jamii kuwa walemavu wasifichwe majumbani na badala yake  wapelekwe hospitalini mapema ili wapate matibabu

Wednesday 2 April 2014

NMB YAINGIA SIHA RASMI

hatimaye Wilaya ya Siha imefanikiwa kupata huduma za kibenki baada ya banki ya NMB kufungua huduma zake katika Wilaya ya Siha

huduma hizi za kibenki zimeanza kutolewa na banki hiyo kuanzia tarehe 25.3.2014 katika mji mdogo wa sanya Juu karibu na barabara inayoelekea ofisi za Halmashauri ya Siha na pembeni mwa Kituo cha mafuta cha Kuringe Petrol station

huduma zinazotolewa na banki hiyo ni pamoja na huduma ya kuweka pesa, huduma ya kutoa pesa,huduma ya kufungua akaunti na Huduma za ATM

Wananchi wa Wilaya ya Siha wamekuwa wakikosa huduma za kibenki kwa muda mrefu sasa na hivyo kuwafanya baadhi ya wananchi kuamua kuweka fedha zao ndani ya nyumba zao au kuchimbia chini jambo ambalo limekuwa likisababisha kuhatarisha maisha yao kwa uvamiwa na watu wabaya.

wananchi wengi wa Wilaya ya siha wanaishukuru Banki ya NMB kuwa mkombozi wao kwa kuwapatia huduma za kibenki karibu na kuwatambua kuwa nao wanastahili kupata huduma hizo ili kuboresha uchumi wa  wananchi wa Siha


HATIMAYE NMB YAINGIA SIHA RASMI

Banki ya NMB imefungua huduma zake katika halmashauri ya wilaya ya siha Kuanzia tarehe 25.03.2014 na kuanza kutoa huduma zake kwa Wananchi wa Wilaya ya Siha

banki hii ambayo imekuwa ya kwanza kufunguliwa katika Wilaya ya Siha tangu kuanzishwa kwa wilaya hiyo mwaka 2007. banki hii ambayo itasaidia Wananchi wa wilaya ya siha kuweza kuhifadhi fedha zao kwa usalama zaidi na kuwaepushia wananchi wa Wilaya ya Siha kero waliyokuwa wanaipata hapo mwanzoniu

huduma zinazotolewa na banki hii ambayo ipo kwa mtindo wa Mobile banki ni pamoja na K

SIHA YAANZISHA GAZETI



Halmashauri ya Wilaya ya Siha inategemea kuanzisha gazeti litakalokuwa linamilikiwa na halmashauri hiyo. lengo la kuanzishwa kwa gazeti hilo ambalo litajulikana kwa jina la SihaLeo ni pamoja na kupanua wigo wa mawasiliano ya umma ya kuwapatia habari wananchi wote wa wilaya ya siha na Mikoa ya kanda ya kaskazini kwa ujumla

Halmashauri hiyo ya Siha kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo inadhamiria kuwapatia wananchi huduma ya upashanaji wa habari ili kukuza dhana ya uwajibikaji na utawala bora katika kuwahudumia wananchi wake

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Siha ndugu Rashid Kitambulio  aliyasema haya wakati aliongea na wanahabari waliomtembelea ofisini kwake juzi walipokuwa wakipata taarifa mbalimbali za utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi ya mwaka 2010.

mkurugenzi huyo alisema kuwa hadi sasa tupo kwenye hatua mbalimbali za kuanzisha na kuzindua gazeti hilo la halmashauri. aliongeza kuwa magazeti yapo mengi lakini gazeti hili liatakuwa na tofauti kubwa kwani litashughulikia mambo ya kijamii zaidi hasa wanaoishi vijijini na maeneo ya pembezoni.

Ndugu Rashid Kitambulio ambaye pia ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Siha ,aliwataka wananchi wa mikoa ya kanda ya kaskazini kujivunia gazeti hilo kwani litakuwa kama alama ya kanda ya kaskazini kwa ajili ya kuwapatia habari na kuwaunganisha wananchi wa jamii mbalimbali wanaishi katika mikoa yote ya kanda ya kaskazini na Tanzania kwa Ujumla.

akizungumza na wanahabari hao katika ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri ya Siha ,Afisa Uhusiano wa Halmashauri hiyo alisema kuwa kama mambo yatakewnda vizuri gazeti hilo litazinduliwa tarehe 26.04.2014 katika maadhimisho ya sherehe za Muungano yanayotegemewa kuadhimishwa  Kimkoa katika Wilaya ya Siha

Ishara na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika Muungano wetu wa miaka 50 ni pamoja na Halmashauri ya siha Kuwa na chombo chake cha kuwapatia wananchi taarifa mbalimbali za maendeleo na kijamii