Thursday, 24 April 2014

WANAFUNZI 42 WAHITIMU KIDATO CHA SITA SANYA DAY


Wanafunzi 42 wamasomo ya sayansi na hisabati  wamehitimu kidato cha sita na kuwa wanafunzi wa kwanza waliosoma katika shule za serikali katika Wilaya ya Siha na kufikia hatua hiyo
Mahafali hayo yaliyofanyika katika shule ya Sekondari Sanya Juu kwa jina maarufu sanya Day yalihudhuriwa pia na wazazi wa wanafunzi hao 42 ndugu jamaa na marafiki wakiwemo wanafunzi wenzao
Mgeni rasmi katika maafali hayo yaliyofanyika leo tarehe 24.04.2014alikuwa ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Siha mheshimiwa Oscar Temi ambaye alifuatana na Wajumbe wengine na baadhi ya wazazi waliowasindikiza watoto wao
Katika mahafali hayo mwenyekiti huyo wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Siha aliwapongeza wanafunzi hao kwa hatua waliyofikia kimasomo na kuwashauri kuwa wasiishie hapo bali waendelee zaidi kimasomo
“Ndugu zangu nimesikia kilio chenu cha muda mrefu cha kukatikiwa na umeme mara kwa mara na hivyo kuwafanya msiweze kutimiza malengo yenu, mimi nitawasaidia kuweka Sola katika darasa moja ili mpake umeme wa kujisomea wakati wote hasa umeme wa kawaida unapoleta shida” mwenyekiti huyo alisema
Shule ya Sekondari Sanya Day ndiyo shule ya pekee  ya Serikali katika Wilaya ya siha yenye wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha Sita na ina jumla ya Wanafunzi 570 kwa sasa

No comments:

Post a Comment