Thursday 8 October 2015

MKUU MPYA WA MKOA WA KILIMANJARO AFANYA ZIARA YA KIKAZI SIHA

 Wakuu wa idara na vitengo Halmashauri ya Siha wakiwa na Mkuu mpya wa Mkoa wa Kilimanjaro Ndg Amos Makala katika ukumbi wa Roman catholic Sanya Juu

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Ndg Amos makala akiwa na baadhi ya wahudumu wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Siha tarehe 01.10.2015 ukumbini Rc
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akiwa na baadhi ya wazee mashuhuri wa Wilaya ya Siha
Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Siha wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ndg Amos Makala katika ziara fupi ya kikazi aliyoifanya Wilaya ya Siha hivi karibuni

MAFURIKO YA MAGUFULI WILAYA YA SIHA

MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CCM NDUGU JOHN POMBE MAGUFULI AKIHUTUBIA MKUTANO WA KAMPENI UWANJA WA CCM ENEO LA SANYA JUU TAREHE 7.10.2015
WANANCHI WALIJITOKEZA KWA WINGI KUMLAKI RAIS MTARAJIWA WA AWAMU YA TANO

Monday 28 September 2015

CHAGUENI VIONGOZI BORA

Mkuu wa Wilaya ya Siha  Dr Charles Mlingwa amewataka Wananchi wa Jimbo la Siha kuchagua viongozi bora na siyo bora viongozi

hayo ameyasema wakati alipokuwa anaongea na Walinzi wa Amani kwa ngazi mbalimbali Wilayani Siha ili kuwakumbusha baadhi ya majukumu wakati huu Nchi inapoelekea katika uchaguzi Mkuu

aliwaambia kuwa amani ya Nchi siyo jambo la kuchezea inatakiwa kulindwa kama mboni ya jicho ,hivyo kila mtu anatakiwa kutambua hilo na kulitenda

aliwaomba Wananchi  kuwachagua viongozi bora kwa ajili ya maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla wake. alisema kuwa tusiwachague viongozi kwa majaribio wala kwa ushabiki bali tunatakiwa kuwachagua viongozi wanaofaa na tuliowazoea na tunaowajua vizuri tabia na mienendo yao

aliwataka Wananchi wa Siha kutokufanya makosa ya kudanganywa na kuchagua viongozi wasiofaa na ambao hatuwafahamu vizuri.
mimi naamini kuwa serikali imefanya mambo mengi sana kwa maendeleo ya Siha na ni budi wananchi kuiunga mkono wakati wa  upigaji  wa kura Oktoba 25 mwaka huu

nawatakia amani iendelee kutawala katika Wilaya yetu ya Siha na Tanzania kwa Ujumla wake, Zaidi ya Wapiga kura elfu Hamsini wanatarajiwa kupiga kura tarehe 25,10. 2015 katika kuchagua viongozi mbalimbali kwa ngazi ya Rais,Mbunge na Madiwani

ZINGATIENI KANUNI NA SHERIA ZA UCHAGUZI 2015

Msimamizi mkuu wa uchaguzi Jimbo la Siha ndg Rashid Kitambulio amewataka wasimamizi wasaidizi kuzingatia sheria na kanuni za uchaguzi ktk zoezi la uchaguzi mkuu Wilayani hapo 2015

msimamizi huyo aliyasema hayo wakati akitoa nasaha na maelekezo ya jinsi ya kufanikisha zoezi hilo muhimu la kitaifa alipokutana na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na walinzi wa amani kwa ngazi ya vijiji na kata

Uchaguzi wa mwaka huu utasaidia kuwapata Madiwani 17 katika kata za Wilaya ya Siha na Mbunge mmoja wa Jimbo la Siha ambapo vyama vilivyoweka wagombea wake kwa ngazi mbalimbali ni pamoja na Chama kinachotawala CCM ,CHADEMA na ACT Wazalendo

TANGAZO LA AJIRA MPYA

HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA

Kumb Na SDC/S.10/2/VOL.III/79                                                      Tarehe: 12/09/2015

TANGAZO  LA  NAFASI  ZA KAZI (LIMERUDIWA)

Mkurugenzi Mtendaji wa  Halmashauri ya Wilaya ya Siha anawatangazia Ajira Watanzania wenye  sifa  za kazi  kama ifuatavyo:-

1) DEREVA  DARAJA LA  II NAFASI 2  (TGOS A):
A: SIFA
i.  Kuajiriwa  wenye cheti cha mtihani  wa kidato cha nne(IV)
ii.  Wenye  leseni daraja  la C ya uendeshaji magari
iii. Wenye uzoefu wa kuendesha magari  kwa muda  usiopungua  miaka  mitatu (3) bila kusababisha ajali.
iv) Wenye  cheti cha majaribio ya ufundi daraja la II.

B:  MAJUKUMU:
i.  Kuendesha  magari ya Abiria  na Malori.
ii. Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote na kufanya uchunguzi  wa gari kabla na  baada ya safari  ili kugundua  ubovu unaohitaji matengenezo.
iii. Kufanya  matengenezo madogomadogo katika gari.
iv. Kutunza    na kuandika daftari  la safari(Log- Book) kwa safari zote.

2)  KATIBU MAHSUSI III - NAFASI MOJA(01)  (TGS B):
A: SIFA
i.   Waombaji wawe na Elimu ya kidato cha nne(Form IV)
ii.  Waombaji wawe  wamehudhuria  mafunzo  ya Uhazili na kufaulu mtihani ya hatua ya tatu.
iii.  Waombaji wawe wamefaulu somo la Hatimkato,  Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja
iv.  Waombaji wawe wamepata mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
v.   Waombaji wawe wamepata cheti katika programu  za Windows,  Microsoft office, Internet, E-Mail na Publisher.
vi.  Mwombaji awe na umri kuanzia miaka  18 – 45.
vii. Weka  picha moja pasport size ya hivi karibuni.
B:  MAJUKUMU:
i.  Kuchapa  barua, taarifa  na nyaraka  za kawaida.
ii. Kusaidia  kupokea  wageni na kuwasaidia  shida zao na kuwaelekeza sehemu  wanapoweza  kushughulikiwa.
iii. Kusaidia kutafuta na kumpatia  Mkuu wake  majalada,nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
iv. Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
v.  Kusaidia kupokea  majalada,  kuyagawa kwa Maafisa   walio sehemu alipo, kuyakusanya, kuyatunza  na kuyarudisha   sehemu husika.

3)  MCHAPA  HATI II -  NAFASI MOJA (1) (TGS B):
A. SIFA:
i.   Mwombaji awe mehitimu kidato cha Nne au Sita.
ii.  Mwombaji awe amefaulu mtihani wa Uhazili hatua ya II kutoka chuo cha Utumishi wa  Umma.
iii.  Mwombaji  awe na ujuzi  wa Kompyuta  hatua  ya I na II kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
iv.   Mwombaji awe na umri kuanzia miaka  18 – 45.
v.    Weka  picha moja pasport size ya hivi karibuni.

B.  MUJUKUMU:
i.  Kuchapa  Taarifa  za  Uthamini na Hati za  Fidia.
ii.  Kuchapa  Nyaraka  na Hati za kumiliki  Ardhi.

4 :  MAELEZO  YA  UJUMLA:
i.     Barua  za  maombi ziandikwe kwa mkono (Hand  writing).
ii.    Mwombaji aonyeshe  wasifu  wake  (CV).
iii.   Barua  za maombi  ziambatishwe  na vivuli vya vyeti vyote.
iv.   Mwombaji awe na umri kuanzia miaka  18 – 45.
v.    Weka  picha moja pasport size ya hivi karibuni.
Vi.   Mwombaji aambatishe  Cheti cha Kuzaliwa.

Mwisho  wa kutuma  maombi ni tarehe : 13/10/2015 saa  9.30  alasiri.

NB: 
Tangazo  hili pia  linapatikana kwenye  tovuti ya  Halmashauri ya Siha, ingia  google andika  www.sihaleo.blog.

Maombi  yote yatumwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji(W),
S.L.P 129,
SANYA JUU  - SIHA

Limetolewa na:

Rashidi  S. Kitambulio
Mkurugenzi Mtendaji(W)
SIHA

Thursday 9 July 2015

ZOEZI LA UANDIKISHAJI LAELEKEA UKINGONI WILAYANI SIHA

BAADHI YA WANANCHI WAKIWA KATKA MSTARI KATIKA SHULE YA MSINGI MAKIWARU KATIKA ZOEZI LA KUPATA VITAMBULISHO VYA MPIGA KURA TAREHE 9.7.2015 WILKAYANI SIHA

Sunday 21 June 2015

WANANCHI WATAKIWA KUJIANDIKISHA

HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA

TANGAZO

AFISA UANDIKISHAJI MKUU  HALMASHAURI (W) SIHA ANAWATANGAZIA WANANCHI WA KATA ZA IVAENY,NASAI,KIRUA NA KASHASHI WILAYANI SIHA KUWA TAREHE 22/6/2015 SAA  12:00 JIONI  NDIYO MWISHO WA ZOEZI LA KUJIANDIKISHA KATIKA KATA TAJWA HAPO JUU

AMEWATAKA WANANCHI WANANCHI KUTUMIA MUDA WA SIKU MOJA ILIYOBAKI YAANI TAREHE 22/6/2015 KUHAKIKISHA KUWA WALE WOTE AMBAO HAWAJAJIANDIKSHA WANAFANYA HIVYO ILI WAPATE NAFASI KUCHAGUA VIONGOZI WANAOWAPENDA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA HUU MWEZI OKTOBA 2015

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA 
RASHID S KITAMBULIO
AFISA UANDIKISHAJI MKUU WILAYANI SIHA

FURSA YA VIWANJA SIHA

 HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA

                                                                                               TAREHE 19/6/2015
T  A  N  G  A  Z  0
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA MKOA WA KILIMANJARO ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE WA TANZANIA KUWA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA INAUZA  VIWANJA  KATIKA  HALMASHAURI YAKE .
VIWANJA HIVI NI VYA MATUMIZI MBALI MBALI NA  BEI YA KIWANJA NI TSHS 2500/= KWA MITA  MOJA  YA MRABA .  VIWANJA HIVI VIPO KATIKA  UWANDA WA JUU WENYE MAZINGIRA MAZURI YENYE HALI BORA KABISA YA HEWA  KUTOKA MLIMA  MREFU BARANIAFRIKA KILIMANJARO
HALMASHAURI YA SIHA INAWAKARIBISHA WALE WOTE WENYE HITAJI LA KIWANJA/VIWANJA KUFIKA OFISI YA MKURUGENZI NA  KUJAZA FOMU ZA MAOMBI.
FOMU ZA MAOMBI  ZINAPATIKANA OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI KWA GHARAMA YA TSHS 20,000/= TU . FOMU  ZIMEANZA KUTOLEWA OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI  WILAYA YA SIHA. FOMU HIZI ZINATAKIWA KUJAZWA NA KURUDISHWA OFISI YA MKURUGENZI MARA BAADA YA KUJAZWA NA RISITI ZITATOLEWA PAPO KWA HAPO
WOTE MNAKARIBISHWA KUPATA VIWANJA KATIKA WILAYA YA SIHA KWANI  NI MIONGONI MWA WILAYA YA MKOA WA KILIMANJARO  YENYE MANDHARI NA HALI YA HEWA YA KUVUTIA,MIONDOMINU BORA, MAJI SAFI NA SALAMA MIONGONI MWA HUDUMA NYINGINE
ISHI WILAYA YA SIHA KWA AFYA BORA NA MAFANIKIO

KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA KWA KUPIGA  SIMU
0655445585 AU
0784445585 AU
0764101535
TANGZO HILI LIMETOLEWA NA
RASHID S. KITAMBULIO MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA -KILIMANJARO