HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA
Kumb Na SDC/S.10/2/VOL.III/79
Tarehe:
12/09/2015
TANGAZO
LA NAFASI ZA KAZI (LIMERUDIWA)
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Siha anawatangazia Ajira Watanzania wenye sifa
za kazi kama ifuatavyo:-
1) DEREVA DARAJA LA
II NAFASI 2 (TGOS A):
A: SIFA
i. Kuajiriwa wenye cheti cha mtihani wa kidato cha nne(IV)
ii. Wenye leseni daraja
la C ya uendeshaji magari
iii. Wenye uzoefu wa kuendesha magari kwa muda
usiopungua miaka mitatu (3) bila kusababisha ajali.
iv) Wenye cheti
cha majaribio ya ufundi daraja la II.
B: MAJUKUMU:
i. Kuendesha magari ya Abiria na Malori.
ii. Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali
nzuri wakati wote na kufanya uchunguzi
wa gari kabla na baada ya
safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo.
iii. Kufanya
matengenezo madogomadogo katika gari.
iv. Kutunza na
kuandika daftari la safari(Log- Book)
kwa safari zote.
2) KATIBU MAHSUSI III - NAFASI MOJA(01) (TGS B):
A: SIFA
i. Waombaji wawe na Elimu ya kidato cha nne(Form
IV)
ii. Waombaji
wawe wamehudhuria mafunzo
ya Uhazili na kufaulu mtihani ya hatua ya tatu.
iii. Waombaji
wawe wamefaulu somo la Hatimkato, Kiswahili
na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja
iv. Waombaji wawe
wamepata mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
v. Waombaji wawe wamepata cheti katika
programu za Windows, Microsoft office, Internet, E-Mail na Publisher.
vi. Mwombaji awe na umri kuanzia
miaka 18 – 45.
vii. Weka picha
moja pasport size ya hivi karibuni.
B: MAJUKUMU:
i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka
za kawaida.
ii. Kusaidia
kupokea wageni na kuwasaidia shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza
kushughulikiwa.
iii. Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake
majalada,nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za
kazi hapo ofisini.
iv. Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi
kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na
wasaidizi hao.
v. Kusaidia kupokea majalada,
kuyagawa kwa Maafisa walio
sehemu alipo, kuyakusanya, kuyatunza na
kuyarudisha sehemu husika.
3) MCHAPA
HATI II - NAFASI MOJA (1) (TGS B):
A. SIFA:
i. Mwombaji awe mehitimu kidato cha Nne au Sita.
ii. Mwombaji awe
amefaulu mtihani wa Uhazili hatua ya II kutoka chuo cha Utumishi wa Umma.
iii.
Mwombaji awe na ujuzi wa Kompyuta
hatua ya I na II kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali.
iv. Mwombaji awe
na umri kuanzia miaka 18 – 45.
v. Weka picha moja pasport size ya hivi karibuni.
B. MUJUKUMU:
i. Kuchapa Taarifa
za Uthamini na Hati za Fidia.
ii. Kuchapa Nyaraka
na Hati za kumiliki Ardhi.
4 :
MAELEZO YA UJUMLA:
i. Barua
za maombi ziandikwe kwa mkono
(Hand writing).
ii. Mwombaji
aonyeshe wasifu wake
(CV).
iii. Barua za maombi
ziambatishwe na vivuli vya vyeti
vyote.
iv. Mwombaji awe
na umri kuanzia miaka 18 – 45.
v. Weka picha moja pasport size ya hivi karibuni.
Vi. Mwombaji
aambatishe Cheti cha Kuzaliwa.
Mwisho wa kutuma
maombi ni tarehe : 13/10/2015 saa
9.30 alasiri.
NB:
Tangazo hili
pia linapatikana kwenye tovuti ya
Halmashauri ya Siha, ingia google
andika www.sihaleo.blog.
Maombi yote
yatumwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji(W),
S.L.P 129,
SANYA JUU - SIHA
Limetolewa na:
Rashidi S. Kitambulio
Mkurugenzi
Mtendaji(W)
SIHA
No comments:
Post a Comment