Monday, 28 September 2015

ZINGATIENI KANUNI NA SHERIA ZA UCHAGUZI 2015

Msimamizi mkuu wa uchaguzi Jimbo la Siha ndg Rashid Kitambulio amewataka wasimamizi wasaidizi kuzingatia sheria na kanuni za uchaguzi ktk zoezi la uchaguzi mkuu Wilayani hapo 2015

msimamizi huyo aliyasema hayo wakati akitoa nasaha na maelekezo ya jinsi ya kufanikisha zoezi hilo muhimu la kitaifa alipokutana na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na walinzi wa amani kwa ngazi ya vijiji na kata

Uchaguzi wa mwaka huu utasaidia kuwapata Madiwani 17 katika kata za Wilaya ya Siha na Mbunge mmoja wa Jimbo la Siha ambapo vyama vilivyoweka wagombea wake kwa ngazi mbalimbali ni pamoja na Chama kinachotawala CCM ,CHADEMA na ACT Wazalendo

No comments:

Post a Comment