Mkuu wa Wilaya ya Siha Dr Charles Mlingwa amewataka Wananchi wa Jimbo la Siha kuchagua viongozi bora na siyo bora viongozi
hayo ameyasema wakati alipokuwa anaongea na Walinzi wa Amani kwa ngazi mbalimbali Wilayani Siha ili kuwakumbusha baadhi ya majukumu wakati huu Nchi inapoelekea katika uchaguzi Mkuu
aliwaambia kuwa amani ya Nchi siyo jambo la kuchezea inatakiwa kulindwa kama mboni ya jicho ,hivyo kila mtu anatakiwa kutambua hilo na kulitenda
aliwaomba Wananchi kuwachagua viongozi bora kwa ajili ya maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla wake. alisema kuwa tusiwachague viongozi kwa majaribio wala kwa ushabiki bali tunatakiwa kuwachagua viongozi wanaofaa na tuliowazoea na tunaowajua vizuri tabia na mienendo yao
aliwataka Wananchi wa Siha kutokufanya makosa ya kudanganywa na kuchagua viongozi wasiofaa na ambao hatuwafahamu vizuri.
mimi naamini kuwa serikali imefanya mambo mengi sana kwa maendeleo ya Siha na ni budi wananchi kuiunga mkono wakati wa upigaji wa kura Oktoba 25 mwaka huu
nawatakia amani iendelee kutawala katika Wilaya yetu ya Siha na Tanzania kwa Ujumla wake, Zaidi ya Wapiga kura elfu Hamsini wanatarajiwa kupiga kura tarehe 25,10. 2015 katika kuchagua viongozi mbalimbali kwa ngazi ya Rais,Mbunge na Madiwani
No comments:
Post a Comment