Thursday 23 March 2017

Tovuti ya Halmashauri ya Siha kuzinduliwa hivi karibuni






Halmashauri ya Wilaya ya Siha inatarajia kuzindua tovuti(website) yake hivi karibuni.lengo la kuzindua tovuti ni kuongeza wigo wa Mawasiliano kwa wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na Nje ya Wilaya ya Siha.
Taarifa zaidi tutaendelea kuwaletea

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano (W)Siha
Tarehe 24.3.2017

Friday 17 March 2017

Madiwani Siha wafundwa kuhusu masuala ya uongozi na maadili

Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Siha wakishiriki katika mafunzo ya siku moja yaliyohusu uongozi na masuala ya utawala bora.mafunzo hayo yamefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha.

Waheshimiwa Madiwani Siha wapata mafunzo ya uongozi na utawala bora

Halmashauri ya wilaya ya Siha yawapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Siha kuhusu masuala ya uongozi,maadili na utawala bora.
Picha za matukio zimeoneshwa hapo chini

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha Valerian Juwal akifungua mafunzo ya siku moja kwa waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Siha.mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika leo tar 17.3.2017 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha
 Afisa wa Serikali za Mitaa mkoa wa Kilimanjaro Grace Makiluli akitoa mada katika mafunzo ya siku moja ya waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Siha
 Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Siha wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha wakisikiliza kwa makini moja ya mada zilizokuwa zinatolewa

Wednesday 15 March 2017

Watendaji wa Kata na Vijiji Halmashauri ya Siha watakiwa kutenda kazi kwa uadilifu



Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Siha akifungua mafunzo kwa watendaji wa Vijiji na Kata zote Halmashauri ya Siha


Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Valerian Juwal amewataka watendaji wa vijiji na Kata kufanya kazi za Umma kwa kuzingatia kanuni,taratibu,miongozo na Sheria za utumishi wa Umma.

Akifungua mafunzo elekezi ya siku mbili katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha , Mkurugenzi  mtendaji wa Halmashauri ya Siha Valerian Juwal aliwataka watendaji wa  vijiji na Kata kuzingatia yale yote yatakayofundishwa kuanzia mwanzo wa mafunzo hadi mwisho wa mafunzo.

Aliwataka watendaji hao kuwa mfano mwema wa kutenda Hali hasa suala la kusimamia ulinzi wa amani pamoja na kusimamia vema ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri katika maeneo yao ya kazi

Aidha ,aliwataka watendaji wa Kata na Vijiji kusimamia agizo la Serikali ya awamo ya tano kuhusu upigwaji marufuku wa matumizi ya madawati ya kulevya pamoja na uuzaji na utumiaji wa pombe za viroba

Nataka kuwaagiza kuwa agizo suala la usimamizi wa Mapato kwa Sasa ni Jambo muhimu sana kwa kila mtu kulichukua na kulifanyia kazi kwa ukaribu zaidi ili kuhakikisha kuwa Mapato ya Serikali hayapotei kwa namna yoyote ile.

Halmashauri ya Wilaya ya Siha inajumla ya Kata 17 na vijiji 60 na Vitongoji 169

Watendaji wa vijiji na kata Wilayani Siha wapata mafunzo elekezi ya kuboresha kazi za Umma

 Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Siha Valerian Juwal  akifungua mafunzo elekezi kwa watendaji wa Kata na Vijiji Halmashauri ya Siha.mafunzo hayo yanafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha kwa muda wa siku mbili tarehe 15.3.2017 hadi tarehe 16.3.2017
Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo watendaji wa Kata na Vijiji vyote Siha ili kuboresha utendaji wa kazi kwa kuzingatia Sheria ,taratibu na kanuni za utumishi wa Umma.
 Afisa wa Serikali za mitaa mkoa wa Kilimanjaro  Grace Makiluli akiendelea kutoa mada ya utendaji wa kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma.watumishi wa umma wametakiwa kutunza siri na Habari za Serikali ovyo ovyo bila kufuata maadili na taratibu za Umma. Katika ngazi ya Halmashauri Mkurugenzi mtendaji ndiye msemaji wa Halmashauri na ngazi ya Wilaya mhe. Mkuu wa Wilaya ndiye msemaji Mkuu kwa ngazi ya Wilaya
Washiriki wa mafunzo hayo wakisikiliza maelekezo kutoka kwa afisa utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Siha kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha muda huu

Tuesday 14 March 2017

Wananchi Wilayani siha washauriwa kufanya mazoezi mara kwa mara

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Siha Valerian Juwal  kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Siha  aliwataka wananchi wa Wilaya ya Siha na watumishi wa  Umma kushiriki vema katika mazoezi ya kila mwezi kama sehemu ya kutii wito wa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliagiza wananchi wote kushiriki mazoezi walau kila jumamosi ya pili ya kila mwezi

Alieleza kuwa Wilaya ya siha imeshazindua siku ya kufanya mazoezi kwa wananchi ambapo uzinduzi huo ulifanyika uwanja wa isanja Nasai. Aliwapongeza wananchi ,watumishi na viongozi wa wananchi walioshiriki vema katika mazoezi hayo na kuwataka kuwa kichocheo kwa wananchi mahali wanakotoka.

Aliongeza kuwa kufanya mazoezi kuna faida nyingi zikiwemo kutunza AFYA bora,kuwa mkakamavu,mchangamvu na mazoezi ya pamoja pia yanasaidia kuongeza mahusiano miongoni mwetu.

Alisema kwa mfano,katika mazoezi tumekuwa pamoja na wenzetu wa Polisi ,Madaktari,wanasiasa,watumishi wa Umma na wananchi wengine pia,kimsingi tumepata fursa ya kujuana na kusalimiana.

Aliongeza kuwa,Halmashauri ya Siha imejipanga kuhakikisha kuwa usimamizi wa mazoezi unakwenda hadi ngazi ya kata na vijiji ili kila mwananchi apate fursa ya kushiriki katika mazoezi kila mwezi.

Aliwataka watendaji wa Kata na Vijiji vyote Siha kuhakikisha kuwa wanapanga utaratibu mzuri kwa kuwashirikisha wananchi kushiriki vema katika mazoezi katika kila kata. Naomba watendaji wangu muwe wabunifu kuchagua eneo katika kata yenu ambayo wananchi watashiriki vema na ikiwezekana kila kijiji wachague  eneo watakaloona linafaa kufanyia mazoezi.

Mwisho Mkurugenzi wa Halmashauri ya Siha kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya aliwataka viongozi wote kushirikiana na Serikali kwa kuwahamasisha wananchi kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuepukana na magonjwa nyemelezi kama vile shinikizo la damu,kisukari na mengine mengi.
 wananchi na watumishi Wilayani Siha wakishiriki katika mazoezi ya pamoja tarehe 11.3.2017 uwanja wa Isanja kata ya Nasai

Mazoezi yakiendelea kwa kasi kubwa siku ya uzinduzi Wilayani Siha

Saturday 11 March 2017

Wilaya ya Siha yazindua siku ya mazoezi kwa kishindo

 Watumishi na wananchi wa Siha wakishiriki mazoezi uwanja wa Isanja leo asubuhi

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha akitoa neno mara baada ya mazoezi
 Watumishi wa Halmashauri ya Siha wakionesha umahiri wao wa kufanya mazoezi

 baadhi ya walioshiriki katika mazoezi ya viunga leo wakifanya aina mbalimbali za mazoezi

 Mhe Juma Jani  (wa tatu kutoka kushoto) Diwani wa kata ya Sanya Juu akishiriki katika siku ya uzinduzi wa mazoezi Wilayani siha tar 11.3.2017
 mhe Robert Mrisho diwani wa kata ya Kirua akionesha umahiri wake katika mazoezi ya viungo  uwanja wa Isanja leo  tar 11.3.2017 asubuhi. Wilaya ya Siha ilizindua siku ya mazoezi kwa wananchi na watumishi wa Umma.

 Watumishi wa Umma,viongozi,na wananchi wakisikiliza maelekezo ya jinsi ya kudumisha utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara
 Hiyo ni sehemu ya mazoezi pia
Mazoezi yakiwa yamekolea na kila mtu alikuwa akifanya aina ya zoezi kulingana na maelekezo

Wednesday 8 March 2017

Ziara ya RC KILIMANJARO Wilayani Siha tarehe 7.3.2017

 Wanafunzi wa Dahani wakijisomea wenyewe katika vikundi mara baada ya muda wa masomo darasani
 RC KILIMANJARO mhe. Saidi Meck Sadiki akikagua ujenzi wa  maabara ya katika Shule ya sekondari Dahani
 Diwani wa kata ya Livishi mhe.Witson Nkini (mbele kushoto) akimuongoza RC KILIMANJARO kukagua ujenzi wa maabara Dahani Sekondari
 Bwawa la Kishisha likiwa na maji kwa ajili ya umwagiliaji. Mfereji  wa Kishisha unaojengwa utapeleka maji ktk bwawa hili
 RC KILIMANJARO akipokea taarifa ya matumizi ya maji katika bwawa la Kishisha
 Wanafunzi wa shule ya sekondari Dahani wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro alipofika shuleni hapo kuangalia maendeleo ya shule
 RC KILIMANJARO(aliyenyanyua mkono) akitoa maelekezo ya jinsi ya kutunza vyanzo vya maji Wilayani Siha.
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akikagua ujenzi wa mfereji wa maji Kishisha
Moja ya  Eneo la mfereji wa maji Kishisha lililokamilika. Jumla ya mita 1000 zinatarajiwa kujengwa mara baada ya awamo ya kwanza inayoendelea kujengwa na mkandarasi wa mfereji huu
 RC akipita katika miteremko mikali ili kukagua mfereji wa maji Kishisha tarehe 7.3.2017
 Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe Onesmo Buswelu (aliyevaa suti nyeusi) aliteremka katika mabonde ili kukagua mfereji wa maji Kishisha

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro mhe. Said Meck Sadikia akipokewa katika ofisi ya DC Siha tarehe 7.3.2017

Tuesday 7 March 2017

DC SIHA apiga marufuku wanafunzi kutumia simu za viganjani

Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Onesmo Buswelu (aliyevaa suti nyeusi katikati) amepiga marufuku wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Wilayani siha kutumia simu za miongoni.

Mkuu huyo wa Wilaya aliyasema hayo katika ziara fupi  ya mhe. Mkuu wa Mkoa wa KILIMANJARO aliyoifanya tarehe 7.3.2017 katika Shule ya sekondari Dahani alipofika kukagua maendeleo ya Elimu katika Shule hiyo.

Alieleza kuwa kuanzia sasa ni marufuku kwa mwanafunzi yeyote wa shule ya msingi na sekondari kumiliki simu za mkononi kwani zinatumika kwa matumizi mabaya ambayo hayahusiani na masomo mashuleni.

Naagiza mwanafunzi yeyote atakayepatikana na simu ya kiganjani mahali popote basi hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya mwanafunzi huyo ikiwa ni pamoja na kumsaka mzazi,mlezi au mtu aliyempa simu mwanafunzi huyo,alisema Buswelu

Kwa upande mwingine Mkuu   wa Wilaya ya Siha aliwataka wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuwa na tabia njema wakiwa shuleni na nyumbani ili kuongeza kiwango cha ufaulu katika Shule wanazosoma.

Alisisitiza kuwa ,nidhamu ndiyo silaha pekee ya ufaulu kwa mwanafunzi , nawaomba watoto wangu muwe na utii kwa walimu na wazazi wenu kama ilivyo Mila na desturi za maadili ya Kitanzania.


Wednesday 1 March 2017

Picha za ziara ya naibu Waziri OR - -TAMISEMI alipotembelea hospital ya Wilaya ya Siha tar 1.3.2017

 Mhe Seleman Jaffo naibu waziri OR - -TAMISEMI akitoa maelekezo katika hospital ya Wilaya ya Siha tar 1.3.2017
 Naibu Waziri OR - -TAMISEMI mhe Seleman Jaffo akiongea na watumishi wa Afya katika hospital ya Wilaya ya Siha alipotembelea hospital hiyo tar 1.3.2017
 Wataalam na viongozi mbalimbali wakimsikiliza mhe Seleman Jaffo naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI alipotembelea hospital ya Wilaya ya Siha tar 1.3.2017
 Mhandisi wa ujenzi Wilaya ya Siha akipokea maelekezo ya kazi kutoka kwa Mhe Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI (mhe Seleman  Jaffo wa pili kutoka kushoto)
 Mhe.Seleman Jaffo naibu waziri OR -TAMISEMI(kwanza kushoto )akipokea maendeleo ya ujenzi wa hospital ya Wilaya ya Siha.
 Jengo mojawapo ya majengo ya hospital ya Wilaya ya Siha lililokuwa kulima na  linayotumika kwa sasa
 Mhe Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI(aliyevaa suti nyeusi kushoto ) akikagua jengo la hospital ya Wilaya ya siha linalotarajiwa kumaliziwa ujenzi wake.serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa Shilingi milioni 250 kukamilisha ujenzi huo

Mhe Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI (aliyesimama) akiongea na watumishi na wananchi waliofika hospitalini hapo kumpokea katika ziara yake ya kukagua ujenzi wa hospital hiyo.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEM atembelea ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Esinyari

 Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI MHE. Seleman Jaffo atembelea shule mpya ya Sekondari Esinyari kata ya Orkolili tar 1.3.2017
 Baadhi ya wah. Madiwani wa Siha wakisalimiana na mhe Seleman Jaffo Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI akiwa na viongozi wa Siha alipokuwa eneo inapojengwa shule mpya ya Sekondari Esinyari
 Mhe. Seleman Jaffo akiagana na baadhi ya viongozi wa Siha wakiwemo wah. Madiwani mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja Wilayani siha tar 1.3.2017
 Mhe. Seleman Jaffo akitoa maelekezo ya kazi alipokuwa katika ziara yake Wilayani Siha tar 1.3.2017
 Mhe.naibu waziri  OR -TAMISEMI akiongea na vyombo vya habari alipotembelea ujenzi wa shule mpya ya Sekondari  Esinyari kata ya Orkolili
 Mtendaji wa Kata ya Orkolili Shedrack Mollel akisoma taarifa ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Esinyari
 Baadhi ya majengo ya shule mpya ya Esinyari kata ya Orkolili Wilayani Siha
 Mhe Seleman Jaffo Naibu waziri OR- TAMISEMI Akifuatilia kwa makini taarifa ya ujenzi wa shule mpya ya Esinyari
Mhe.Seleman Jaffo naibu waziri OR TAMISEMI akiagana na baadhi ya wahemiwa Madiwani wa Halmashauri ya Siha katika kituo cha Mabasi Orkolili - KIA