Tuesday 7 March 2017

DC SIHA apiga marufuku wanafunzi kutumia simu za viganjani

Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Onesmo Buswelu (aliyevaa suti nyeusi katikati) amepiga marufuku wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Wilayani siha kutumia simu za miongoni.

Mkuu huyo wa Wilaya aliyasema hayo katika ziara fupi  ya mhe. Mkuu wa Mkoa wa KILIMANJARO aliyoifanya tarehe 7.3.2017 katika Shule ya sekondari Dahani alipofika kukagua maendeleo ya Elimu katika Shule hiyo.

Alieleza kuwa kuanzia sasa ni marufuku kwa mwanafunzi yeyote wa shule ya msingi na sekondari kumiliki simu za mkononi kwani zinatumika kwa matumizi mabaya ambayo hayahusiani na masomo mashuleni.

Naagiza mwanafunzi yeyote atakayepatikana na simu ya kiganjani mahali popote basi hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya mwanafunzi huyo ikiwa ni pamoja na kumsaka mzazi,mlezi au mtu aliyempa simu mwanafunzi huyo,alisema Buswelu

Kwa upande mwingine Mkuu   wa Wilaya ya Siha aliwataka wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuwa na tabia njema wakiwa shuleni na nyumbani ili kuongeza kiwango cha ufaulu katika Shule wanazosoma.

Alisisitiza kuwa ,nidhamu ndiyo silaha pekee ya ufaulu kwa mwanafunzi , nawaomba watoto wangu muwe na utii kwa walimu na wazazi wenu kama ilivyo Mila na desturi za maadili ya Kitanzania.


No comments:

Post a Comment