Monday 24 March 2014

WANANCHI SIHA WANUFAIKA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII



Shirika lisilo la kiserikali FARM ACCESS kutoka nchini Uholanzi limeonyesha dhamira ya dhati katika kuboresha afya ya wananchi wote wa wilaya ya siha kupitia mfuko wa afya ya jamii(CHF).

Hayo yalisemwa na meneja wa mradi huo ndugu Henri Maro katika moja ya mafunzo yaliyotolewa na shirika hilo kwa watendaji mbalimbali Wilayani Siha yaliyokuwa na malengo ya kuongeza uelewa kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko huo kwa umma

Dr. Best Magoma Mkuu wa Idara ya Afya katika Halmashauri ya Siha kabla ya kumkaribisha  mkurugenzi mtendaji  alisema kuwa mfuko wa afya ya jamii Wilayani Siha ulianza mwaka 2012 kupitia chama cha wakulima wa kahawa KNCU.Aliongeza kuwa hadi sasa mwaka wa 2014 mfuko una wanachama zaidi ya kaya 1400 katika wilaya ya siha. Aliongeza kuwa huduma hizi zitatolewa katika hospital za umma,binafsi na za mashirika ya dini pia

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha ndugu Rashid Kitambulio  kwa upande wake aliwashukuru wawakilishi wa shirika la FARM ACCESS Kwa kuichagua Wilaya ya siha kuwa miongoni mwa Wilaya chache za Tanzania zilizoonyesha nia na dhamira ya kweli katika kuboresha afya ya wananchi wake.


Katika hotuba yake fupi mkurugenzi wa siha aliawaomba wananchi  kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha zoezi hilo lenye manufaa kwa wananchi wa kawaida hasa wale wasio na sekta rasmi hasa waishio vijijini.

Wilaya ya Siha imeweka malengo ya kufikia asilimia 30 ya kaya zote zilizopo wilayani siha hadi ifikapo mwaka wa 2015. Mfuko huu wa afya ya jamii utasaidia kuboresha afya za wananchi wa wilaya ya Siha kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na mifuko mingine inayojali watumishi wa umma pekee.





SIHA YAPATA WALIMU ZAIDI YA 145

Halmashauri ya wilaya ya siha imepata walimu wa ajira mpya zaidi ya 145 kwa shule za msingi na sekondari kwa mwaka wa 2014
Hayo yalisemwa na wakuu wa idara za elimu msingi ndg Rose Sandi na Abraham Kanji mkuu wa idara ya elimu sekondari wote wawili walisema kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji
wilaya ya siha imejipanga vema kuwapokea walimu waliopangwa katika wilaya ya siha ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa na kuwa na mwanzo mzuri
kati ya walimu hawa waliopangwa wilaya ya siha ,walimu 113 ni wa shule za sekondari na zaidi ya walimu 34 ni wa shule za msingi. walimu hawa watasaidia kupunguza upungufu wa walimu na kuongeza ufaulu wa kitaaluma unakuwa siku hadi siku katika wilaya ya siha. wilaya ya siha ina jumla ya shule 13 za sekondari zinazomilikiwa na serikali na shule 54 za msingi zinazomilikiwa na serikali pia.

wilaya ya siha ni wilaya yenye mazingira mazuri ya kufanyia kazi na huduma zote za muhimu zinapatikana katika maeneo yote ya wilaya ya siha kama vile maji safi na salama,umeme,barabara na mawasiliano ya uhakika