Shirika
lisilo la kiserikali FARM ACCESS kutoka nchini Uholanzi limeonyesha dhamira ya
dhati katika kuboresha afya ya wananchi wote wa wilaya ya siha kupitia mfuko wa
afya ya jamii(CHF).
Hayo
yalisemwa na meneja wa mradi huo ndugu Henri Maro katika moja ya mafunzo
yaliyotolewa na shirika hilo kwa watendaji mbalimbali Wilayani Siha yaliyokuwa
na malengo ya kuongeza uelewa kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko huo kwa umma
Dr.
Best Magoma Mkuu wa Idara ya Afya katika Halmashauri ya Siha kabla ya
kumkaribisha mkurugenzi mtendaji alisema kuwa mfuko wa afya ya jamii Wilayani
Siha ulianza mwaka 2012 kupitia chama cha wakulima wa kahawa KNCU.Aliongeza
kuwa hadi sasa mwaka wa 2014 mfuko una wanachama zaidi ya kaya 1400 katika
wilaya ya siha. Aliongeza kuwa huduma hizi zitatolewa katika hospital za
umma,binafsi na za mashirika ya dini pia
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Siha ndugu Rashid Kitambulio kwa upande wake aliwashukuru wawakilishi wa
shirika la FARM ACCESS Kwa kuichagua Wilaya ya siha kuwa miongoni mwa Wilaya
chache za Tanzania zilizoonyesha nia na dhamira ya kweli katika kuboresha afya
ya wananchi wake.
Katika
hotuba yake fupi mkurugenzi wa siha aliawaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha
zoezi hilo lenye manufaa kwa wananchi wa kawaida hasa wale wasio na sekta rasmi
hasa waishio vijijini.
Wilaya
ya Siha imeweka malengo ya kufikia asilimia 30 ya kaya zote zilizopo wilayani
siha hadi ifikapo mwaka wa 2015. Mfuko huu wa afya ya jamii utasaidia kuboresha
afya za wananchi wa wilaya ya Siha kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na mifuko
mingine inayojali watumishi wa umma pekee.
No comments:
Post a Comment