Wednesday 2 April 2014

SIHA YAANZISHA GAZETI



Halmashauri ya Wilaya ya Siha inategemea kuanzisha gazeti litakalokuwa linamilikiwa na halmashauri hiyo. lengo la kuanzishwa kwa gazeti hilo ambalo litajulikana kwa jina la SihaLeo ni pamoja na kupanua wigo wa mawasiliano ya umma ya kuwapatia habari wananchi wote wa wilaya ya siha na Mikoa ya kanda ya kaskazini kwa ujumla

Halmashauri hiyo ya Siha kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo inadhamiria kuwapatia wananchi huduma ya upashanaji wa habari ili kukuza dhana ya uwajibikaji na utawala bora katika kuwahudumia wananchi wake

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Siha ndugu Rashid Kitambulio  aliyasema haya wakati aliongea na wanahabari waliomtembelea ofisini kwake juzi walipokuwa wakipata taarifa mbalimbali za utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi ya mwaka 2010.

mkurugenzi huyo alisema kuwa hadi sasa tupo kwenye hatua mbalimbali za kuanzisha na kuzindua gazeti hilo la halmashauri. aliongeza kuwa magazeti yapo mengi lakini gazeti hili liatakuwa na tofauti kubwa kwani litashughulikia mambo ya kijamii zaidi hasa wanaoishi vijijini na maeneo ya pembezoni.

Ndugu Rashid Kitambulio ambaye pia ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Siha ,aliwataka wananchi wa mikoa ya kanda ya kaskazini kujivunia gazeti hilo kwani litakuwa kama alama ya kanda ya kaskazini kwa ajili ya kuwapatia habari na kuwaunganisha wananchi wa jamii mbalimbali wanaishi katika mikoa yote ya kanda ya kaskazini na Tanzania kwa Ujumla.

akizungumza na wanahabari hao katika ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri ya Siha ,Afisa Uhusiano wa Halmashauri hiyo alisema kuwa kama mambo yatakewnda vizuri gazeti hilo litazinduliwa tarehe 26.04.2014 katika maadhimisho ya sherehe za Muungano yanayotegemewa kuadhimishwa  Kimkoa katika Wilaya ya Siha

Ishara na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika Muungano wetu wa miaka 50 ni pamoja na Halmashauri ya siha Kuwa na chombo chake cha kuwapatia wananchi taarifa mbalimbali za maendeleo na kijamii

2 comments: