Shirika lisilo la
kiserikali (CCBRT) tawi la Moshi leo limetoa huduma zake katika halmashauri ya
wilaya ya siha katika Jengo jipya la Hospital ya Wilaya ya Siha lililopo karibu
na mji mdogo wa sanya Juu
Shirika hilo lenye makao
yake makuu Dar es salaam na lina tawi lake kubwa katika mji wa Moshi eneo la
kaloleni Pasua leo limetoa huduma mbalimbali za kuwachunguza na kuwapatia
matibabu na hasa ushauri kwa walezi wa walemavu ambao leo walifurika kwa wingi
katika jingo hilo jipya la Hospital ya wilaya ya Siha
Mkurugenzi wa CCBRT tawi la Moshi alisema kuwa
baadhi ya huduma ambazo zinatolewa na shirika hilo kwa watoto wenye umri chini ya miaka 18 na
wanawake ni pamoja na watoto wenye matatizo ya Mpasuko wa mdomo(cleft Lip),Kuvuja
mkojo kwa wanawake baada ya kujifungua(VVF),miguu iliyopinda kwenye nyayo
Ruth Mlay mkurugenzi wa
CCBRT-Moshi aliongeza kuwa mbali na huduma hizo pia wanatoa huduma kwa watoto
wenye mtindio wa ubongo(cerebral Palsy),watoto wenye uvimbe Mgongoni(spina
Bifida) na pia watoto wenye kichwa kikubwa (Hydrochephalus)
Akiongea katika shughuli
hiyo Daktari Mkuu wa Wilaya ya Siha Dr
Best Magoma alisema kuwa jambo la kwanza walilolifanya ni kuwagundua walemavu
wote katika Wilaya ya siha na maeneo wanayotoka. Alisema kuwa anawashukuru
Wananchi wote wa Siha kwa kuitikia wito na kutoa ushirikiano wa kutosha hadi
zoezi hili zimefankiwa kwa kiasi kikubwa
Pia Dr Best magoma
aliwashukuru viongozi wa taasisi mbalimbali hasa taasisi za dini ambazo alisema
zimetoa ushirikiano mkubwa sana wa kuhamasisha jamii hasa za vijijini kwa ajili
ya kufanikisha kazi hii kubwa na yenye manufaa kwa jamii. Alisema kuwa Wilaya
ya Siha hadi sasa inajumla ya walemavu mbalimbali wapatao 552 wenye ulemavu wa
aina mbalimbali
Mkuu huyo wa Idara ya afya
katika Wilaya ya Siha aliongeza kuwa walemavu wanayo haki ya kuishi na
kujitegemea iwapo jamii itawajea uwezo badala ya kuwafungia ndani na kuwaona
kama ni mkosi katika familia. Aliomba jamii kubadilika sasa na kuondokana na
dhana potofu ya kuwatenga walemavu katika shughuli za kijamii
Afisa ustawi wa jamii ndugu
Peter Msaka akiongea katika zoezi hilo alisema kuwa bado elimu zaidi
inahitajika kwa jamii ili kuweza kuondokana na mila zisizo na maana za
kuwatenga na kuwadharau walemavu katika jamii. Alitoa wito kwa jamii kuwa
walemavu wasifichwe majumbani na badala yake wapelekwe hospitalini mapema ili wapate
matibabu
No comments:
Post a Comment