hatimaye Wilaya ya Siha imefanikiwa kupata huduma za kibenki baada ya banki ya NMB kufungua huduma zake katika Wilaya ya Siha
huduma hizi za kibenki zimeanza kutolewa na banki hiyo kuanzia tarehe 25.3.2014 katika mji mdogo wa sanya Juu karibu na barabara inayoelekea ofisi za Halmashauri ya Siha na pembeni mwa Kituo cha mafuta cha Kuringe Petrol station
huduma zinazotolewa na banki hiyo ni pamoja na huduma ya kuweka pesa, huduma ya kutoa pesa,huduma ya kufungua akaunti na Huduma za ATM
Wananchi wa Wilaya ya Siha wamekuwa wakikosa huduma za kibenki kwa muda mrefu sasa na hivyo kuwafanya baadhi ya wananchi kuamua kuweka fedha zao ndani ya nyumba zao au kuchimbia chini jambo ambalo limekuwa likisababisha kuhatarisha maisha yao kwa uvamiwa na watu wabaya.
wananchi wengi wa Wilaya ya siha wanaishukuru Banki ya NMB kuwa mkombozi wao kwa kuwapatia huduma za kibenki karibu na kuwatambua kuwa nao wanastahili kupata huduma hizo ili kuboresha uchumi wa wananchi wa Siha
NMB manjulikana kama wakombozi wa wanyonge
ReplyDeleteHII NI HABARI NJEMA KWA MAENDELEO YA WILAYA YA SIHA. AWALI WATUMISHI NA WANANCHI WENGINE WALIKUWA WANATUMIA BENKI YA WILAYA JIRANI AMBAPO MATUMIZI YA AWALI YALIFANYIKA WILAYANI HUMO NA HIVYO KUFIFISHA MAENDELEO YA SIHA.
ReplyDeleteKWASASA MZUNGUKO WA FEDHA UTAKUWA NDANI YA WILAYA. JITIHADA ZIENDELEE ZA KUZISHAWISHI BENKI NYINGINE KUWEKEZA SIHA PIA.
SIHA OYEEEEE!