Monday 28 September 2015

TANGAZO LA AJIRA MPYA



HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA


Kumb Na SDC/S.10/2/VOL.III/79                                                      Tarehe: 12/09/2015


TANGAZO  LA  NAFASI  ZA KAZI (LIMERUDIWA)

Mkurugenzi Mtendaji wa  Halmashauri ya Wilaya ya Siha anawatangazia Ajira Watanzania wenye  sifa  za kazi  kama ifuatavyo:-

1) DEREVA  DARAJA LA  II NAFASI 2  (TGOS A):
A: SIFA
i.  Kuajiriwa  wenye cheti cha mtihani  wa kidato cha nne(IV)
ii.  Wenye  leseni daraja  la C ya uendeshaji magari
iii. Wenye uzoefu wa kuendesha magari  kwa muda  usiopungua  miaka  mitatu (3) bila kusababisha ajali.
iv) Wenye  cheti cha majaribio ya ufundi daraja la II.

B:  MAJUKUMU:
i.  Kuendesha  magari ya Abiria  na Malori.
ii. Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote na kufanya uchunguzi  wa gari kabla na  baada ya safari  ili kugundua  ubovu unaohitaji matengenezo.
iii. Kufanya  matengenezo madogomadogo katika gari.
iv. Kutunza    na kuandika daftari  la safari(Log- Book) kwa safari zote.

2)  KATIBU MAHSUSI III - NAFASI MOJA(01)  (TGS B):
A: SIFA
i.   Waombaji wawe na Elimu ya kidato cha nne(Form IV)
ii.  Waombaji wawe  wamehudhuria  mafunzo  ya Uhazili na kufaulu mtihani ya hatua ya tatu.
iii.  Waombaji wawe wamefaulu somo la Hatimkato,  Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja
iv.  Waombaji wawe wamepata mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
v.   Waombaji wawe wamepata cheti katika programu  za Windows,  Microsoft office, Internet, E-Mail na Publisher.
vi.  Mwombaji awe na umri kuanzia miaka  18 – 45.
vii. Weka  picha moja pasport size ya hivi karibuni.
B:  MAJUKUMU:
i.  Kuchapa  barua, taarifa  na nyaraka  za kawaida.
ii. Kusaidia  kupokea  wageni na kuwasaidia  shida zao na kuwaelekeza sehemu  wanapoweza  kushughulikiwa.
iii. Kusaidia kutafuta na kumpatia  Mkuu wake  majalada,nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
iv. Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
v.  Kusaidia kupokea  majalada,  kuyagawa kwa Maafisa   walio sehemu alipo, kuyakusanya, kuyatunza  na kuyarudisha   sehemu husika.


3)  MCHAPA  HATI II -  NAFASI MOJA (1) (TGS B):
A. SIFA:
i.   Mwombaji awe mehitimu kidato cha Nne au Sita.
ii.  Mwombaji awe amefaulu mtihani wa Uhazili hatua ya II kutoka chuo cha Utumishi wa  Umma.
iii.  Mwombaji  awe na ujuzi  wa Kompyuta  hatua  ya I na II kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
iv.   Mwombaji awe na umri kuanzia miaka  18 – 45.
v.    Weka  picha moja pasport size ya hivi karibuni.

B.  MUJUKUMU:
i.  Kuchapa  Taarifa  za  Uthamini na Hati za  Fidia.
ii.  Kuchapa  Nyaraka  na Hati za kumiliki  Ardhi.

4 :  MAELEZO  YA  UJUMLA:
i.     Barua  za  maombi ziandikwe kwa mkono (Hand  writing).
ii.    Mwombaji aonyeshe  wasifu  wake  (CV).
iii.   Barua  za maombi  ziambatishwe  na vivuli vya vyeti vyote.
iv.   Mwombaji awe na umri kuanzia miaka  18 – 45.
v.    Weka  picha moja pasport size ya hivi karibuni.
Vi.   Mwombaji aambatishe  Cheti cha Kuzaliwa.

Mwisho  wa kutuma  maombi ni tarehe : 13/10/2015 saa  9.30  alasiri.

NB: 
Tangazo  hili pia  linapatikana kwenye  tovuti ya  Halmashauri ya Siha, ingia  google andika  www.sihaleo.blog.

Maombi  yote yatumwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji(W),
S.L.P 129,
SANYA JUU  - SIHA

Limetolewa na:


Rashidi  S. Kitambulio
Mkurugenzi Mtendaji(W)
SIHA

No comments:

Post a Comment