Sunday 21 June 2015

FURSA YA VIWANJA SIHA




 HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA


                                                                                               TAREHE 19/6/2015
T  A  N  G  A  Z  0
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA MKOA WA KILIMANJARO ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE WA TANZANIA KUWA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA INAUZA  VIWANJA  KATIKA  HALMASHAURI YAKE .
VIWANJA HIVI NI VYA MATUMIZI MBALI MBALI NA  BEI YA KIWANJA NI TSHS 2500/= KWA MITA  MOJA  YA MRABA .  VIWANJA HIVI VIPO KATIKA  UWANDA WA JUU WENYE MAZINGIRA MAZURI YENYE HALI BORA KABISA YA HEWA  KUTOKA MLIMA  MREFU BARANIAFRIKA KILIMANJARO
HALMASHAURI YA SIHA INAWAKARIBISHA WALE WOTE WENYE HITAJI LA KIWANJA/VIWANJA KUFIKA OFISI YA MKURUGENZI NA  KUJAZA FOMU ZA MAOMBI.
FOMU ZA MAOMBI  ZINAPATIKANA OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI KWA GHARAMA YA TSHS 20,000/= TU . FOMU  ZIMEANZA KUTOLEWA OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI  WILAYA YA SIHA. FOMU HIZI ZINATAKIWA KUJAZWA NA KURUDISHWA OFISI YA MKURUGENZI MARA BAADA YA KUJAZWA NA RISITI ZITATOLEWA PAPO KWA HAPO
WOTE MNAKARIBISHWA KUPATA VIWANJA KATIKA WILAYA YA SIHA KWANI  NI MIONGONI MWA WILAYA YA MKOA WA KILIMANJARO  YENYE MANDHARI NA HALI YA HEWA YA KUVUTIA,MIONDOMINU BORA, MAJI SAFI NA SALAMA MIONGONI MWA HUDUMA NYINGINE
ISHI WILAYA YA SIHA KWA AFYA BORA NA MAFANIKIO

KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA KWA KUPIGA  SIMU
0655445585 AU
0784445585 AU
0764101535
TANGZO HILI LIMETOLEWA NA
RASHID S. KITAMBULIO MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA -KILIMANJARO

No comments:

Post a Comment