Friday, 5 June 2015

SIHA YAPATA KIJIJI BORA KWA USAFI WA MAZINGIRA


KIJIJI CHA MAWASILIANO CHASHIKA NAFASI YA 3 KWA USAFI TANZANIA

Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro imezidi kutia fora katika siku ya Mazingira Duniani iliyoazimishwa jijini Tanga baada ya kijiji cha MAWASILIANO kata ya Gararagua kushika nafasi ya Tatu kwa vijiji visafi kabisa Tanzania bara na kuziacha Wilaya Kongwe hapa Nchini  zikishangaa mafanikio hayo.Kijiji cha kwanza Tanzania ni Sorera-Kondoa namba mbili ni kijiji cha Image-Njombe

Mafanikio ya Kijiji cha Mawasiliano yametokana na ushirikiano mkubwa kati ya Wananchi wa kata ya Gararagua,Viongozi wote wa Kijiji,na Vitongoji pamoja na uongozi mzima wa Wilaya ya Siha

"SIHA MBELE DAIMA"

1 comment: