Tume ya taifa ya Uchaguzi imesogeza mbele zoezi la uandikishaji ambalo lilikua lianze tarehe 09/06/2015 Mkoa wa Kilimanjaro na Badala yake zoezi hilo litaanza tarehe 16/06/2015
Wananchi wametakiwa kujitokeza kwa Wingi wakati zoezi hilo litakapoanza rasmi tarehe 16/06/2015 na kuepukana na propaganda kuwa zoezi hilo linaendelea kwa sasa katika maeneo mbalimbali Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha ambaye ni msimamizi mkuu wa zoezi hilo Wilayani Siha amewataka Wananchi kutulia na Kusubiri tarehe iliyopangwa na tume ifike na amewahakikishia Wananchi wa Siha kuwa wasihofu kwani Watu wote wataandikishwe katika Wilaya ya Siha kwa kuzingatia Taratibu na Sheria za Uandikishaji
No comments:
Post a Comment