Friday, 5 June 2015

WANANCHI WA SIHA WATAKIWA KUJITOKEZA KATIKA ZOEZI LA KUJIANDIKISHA KWA UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU





                       
                                                                                                               TAREHE 05.6.2015

TANGAZO KWA UMMA
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE WA WILAYA YA SIHA WENYE UMRI WA MIAKA 18 AU ZAIDI KUWA,ZOEZI LA UANDIKISHAJI KWA AJILI YA KUPIGA KURA UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU LITAANZA TAREHE 12/06/2015 HADI TAREHE 12/7/2015.

WANANCHI WOTE WENYE SIFA  MNATAKIWA KUTUMIA MUDA ULIOPANGWA WA KUJIANDIKISHA VIZURI ILI MUWEZE KUTUMIA HAKI YENU YA KIDEMOKRASIA YA KUCHAGUA VIONGOZI MNAOWATAKA KWA AJILI YA MAENDELEO YA WILAYA YA SIHA
NAWATAKIA MAFANIKIO MEMA KATIKA ZOEZI HILI MUHIMU

LIMETOLEWA NA
RASHID S KITAMBULIO
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
SIHA

No comments:

Post a Comment