Mafanikio
ya Halmshauri ya Siha Sekta Barabara 2015-2020
Katika kipindi cha
miaka mitano Halmasauri ya Siha imepokea kiasi cha shilingi 57.2 bilioni kutoka
Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi na ukarabati a miundombinu ya barabara kwa kiwango
cha lami,changarawe na ukarabati wa
barabara vijijini.
Fedha zilizotolewa na
Serikali ya Tanzania zimesaidia ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa km
32.2 kutoka Sanya Juu hadi Elerai,ujenzi wa barabara za changarawe vijijini jumla
ya km 199.2.
Pia Serikali ya awamu
ya tano chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Dkt. John
Magufuli imewezesha Madaraja muhimu kama
vile Kisube kirisha, Lawate loiwang, Muri - Nkwamariko na
Mwaru.
Aidha,Serikali
ya Tanzania kupitia wakala wa Barabara TARURA imefanikiwa kufanya ukarabati wa barabara
zenye urefu wa km 236.81 na kuifanya
halmashauri ya Siha kuwa miongoni mwa Halmashauri hapa nchini zenye barabara
zinazopitika wakati wote wa mwaka.
Mafanikio
haya yote yametokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Serikali na Wananchi wa
Wilaya ya Siha pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya
Wilaya.
No comments:
Post a Comment