Friday, 18 September 2020

 

Mafanikio ya Halmshauri ya Siha Sekta Barabara 2015-2020

Katika kipindi cha miaka mitano Halmasauri ya Siha imepokea kiasi cha shilingi 57.2 bilioni kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi na ukarabati a miundombinu ya barabara kwa kiwango  cha lami,changarawe na ukarabati wa barabara vijijini.

Fedha zilizotolewa na Serikali ya Tanzania zimesaidia ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa km 32.2 kutoka Sanya Juu hadi Elerai,ujenzi wa barabara za changarawe vijijini jumla ya km 199.2.

Pia Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Dkt. John Magufuli  imewezesha Madaraja muhimu kama vile  Kisube kirisha, Lawate loiwang, Muri - Nkwamariko na Mwaru.

Aidha,Serikali ya Tanzania kupitia wakala wa Barabara TARURA imefanikiwa kufanya ukarabati wa barabara zenye urefu wa km 236.81 na kuifanya halmashauri ya Siha kuwa miongoni mwa Halmashauri hapa nchini zenye barabara zinazopitika wakati wote wa mwaka.

Mafanikio haya yote yametokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Serikali na Wananchi wa Wilaya ya Siha pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya Wilaya.

No comments:

Post a Comment