Halmashauri ya Siha yapongezwa na kuboresha stendi ya mabasi Sanya Juuu
Wakazi na Wananchi wa Wilaya ya Siha wameendelea kutoa pongezi kwa Halmashauri ya Siha kwa kuboresha kituo cha Mabasi Sanya Juu. Wanachi hao hasa madereva na wamiliki wa magari ya abiria katika nyakati tofauti wameeleza kufurahishwa na miundombinu bora na imara iliyopo katika stendi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha ndugu Ndaki Mhuli akiwa na viongozi wa dini hivi karibuni ambapo walitembelea stendi hiyo alieleza kuwa Halmashauri ya Siha imetumia zaidi ya shilingi Milioni 4 ya mapato ya ndani katika kuboresha miundombinu ya Stendi ya Sanya Juu na ile ya KIA.
No comments:
Post a Comment