Friday 12 May 2017

Serikali Wilaya ya Siha kuboresha miundombinu ya soko Sanya Juu

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa  jumla ya fedha za kitanzania milioni  71  ili kuboresha miundombinu katika soko la Sanya Juu Wilayani Siha.

Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe.Onesmo Buswelu akitoa taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyasema hayo leo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha.

Alieleza kuwa kazi hiyo inatarajiwa kuanza hivi karibuni na kutaka taratibu na kuanza kazi hiyo zifanyike kwa haraka na kwa kuzingatia taratibu zilizopo ili kuepukana makosa na hoja mbalimbali za ukaguzi.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha kuhakikisha kuwa fedha zilizotolewa na Serikali zinatumika vizuri ili kutoa thamani halisi ya fedha hizo.

Kukamilika kwa ujenzi wa soko hilo kutasaidia kuondoa adha na changamoto mbalimbali zilizopo katika soko hilo hasa nyakati za mvua nyingi kama ilivyo sasa.

No comments:

Post a Comment