Wednesday 24 May 2017

TAARIFA KWA UMMA



OFISI YA RAIS TAMISEMI
                             HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA

   
TAARIFA KWA UMMA 

Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro inapenda kuujulisha Umma kuwa taarifa iliyotolewa na gazeti la Nipashe la tarehe 23 Mei,2017 yenye kichwa cha maneno “Viwanja Vyageuzwa Mashamba Kodi”
 
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Siha inapenda kuufahamisha Umma kuwa taarifa iliyotolewa siyo sahihi na ilikuwa na lengo la kuupotosha Umma na kuwapa hofu wanaomiliki viwanja Siha. Ukweli wa jambo hili ni kuwa eneo lililokodishwa na Halmashauri  lenye ukubwa wa hekari 767 siyo eneo la  viwanja kama ilivyoandikwa na gazeti tajwa hapo juu, bali eneo hili lilitengwa na Halmashauri ya Siha kwa ajili ya shughuli za uwekezaji. 

Aidha,Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Siha inapenda kufahamisha Wananchi wote wanaomiliki viwanja vilivyopimwa  katika Halmashauri ya Siha kuwa viwanja vyao vipo salama na Halmashauri haijawahi kubadilisha matumizi ya ardhi hiyo.

Hata hivyo,Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Siha inatoa wito kwa Wananchi wote wanaomiliki viwanja katika eneo la Halmashauri kuviendeleza viwanja wanavyomiliki.

 Imetolewa na:-

Zakayo Elifaison
Mkuu wa Kitengo cha Habari & Mawasiliano Halmashauri (W) Siha
24 Mei, 2017









No comments:

Post a Comment