Mkuu wa Wilaya ya Siha
Mhe.Onesmo Buswelu awataka wanaomiliki mashamba kwa ajili ya kilimo cha kahawa
kuyaendeleza mashamba hayo kwa mujibu wa mikataba yao kabla ya Serikali
haijawachukulia hatua za Kisheria ikiwa ni pamoja na kuyachukua mashamba hayo.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema hayo
katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha leo tarehe 15.5.2017 alipokuwa
akiongea na Wakulima na Wamiliki ya mashamba yanayoendesha kilimo cha Kahawa
Wilayani Siha.
Mhe. Onesmo Buswelu aliwataka
maofisa ugani wote pamoja na vyama vya ushirika kuhakikisha kuwa vinawapatia
wananchi elimu ya kutosha kuhusu utunzaji wa zao la kahawa kwani ndiyo zao la
kiuchumi linaloweza kuwakomboa Wananchi katika umaskini wa kipato kama ilivyokuwa
hapo miaka1960 na 1970.
Aliwataka wanunuzi binafsi
kutoa bei nzuri kwa wakulima na kuacha tabia za kuwanyonya Wakulima kwa kuwapa bei za chini ambazo kimsingi ndizo
zinawakatisha tamaa ya kulima zao hilo.
Mhe. Onesmo Buswelu Mkuu wa
Wilaya ya Siha ametoa wito kwa Wananchi
wa Siha kutumia vema mvua zinazoendelea kunyesha katika kupanda mazao ya kudumu
kama vile zao la Kahawa ,Matunda na mazao mengine kwa faida ya kizazi cha sasa
na baadaye.
No comments:
Post a Comment