Wednesday 24 May 2017

Milioni 36 kutolewa kwa Wanawake Siha



Halmashauri ya Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro inatarajia kutoa zaidi ya Shilingi milioni 36 kwa ajili ya mikopo ya Wanawake Wilayani hapa.

Jumla ya vikundi 12 vyenye wanufaika 249 vinatarajiwa kufaidika  na fedha hizo zinazotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Siha. Fedha zinazotolewa  na Halmashauri ya Wilaya ya Siha  ni sehemu ya ya  asilimia 5 ya  Mapato ya ndani  ya Halmashauri.

Mwezi Agosti katika mwaka huu wa fedha 2016/2017 Halmashauri ya Wilaya ya Siha ilitoa Mikopo kwa vikundi 10 vya Wanawake Wilayani Siha vilivyokuwa na wanufaika 157 yenye thamani ya Shilingi milioni 20 ambapo kila kikundi kilipatiwa mkopo wa Shilingi milioni mbili.

Halmashauri ya Wilaya ya Siha katika utekelezaji wa bajeti yake kila mwaka  imekuwa ikitenga asilimia 5 ya Mapato ya ndani kwa ajili ya Mikopo ya Wanawake na asilimia 5 kwa ajili ya Vijana.

No comments:

Post a Comment