Wilaya ya
Siha Mkoa wa Kilimanjaro inahitaji walimu 54 wa masomo ya Hisabati na Sayansi
kwa shule za Sekondari za Serikali.
Akitoa
taarifa ya maendeleo ya shule kwa Mkuu wa Wilaya ya Siha,Mkuu wa shule ya
Sekondari Fuka Mwalimu Swalehe Kombo alieleza
kuwa Shule yake inahitaji kubwa la walimu wa Sayansi na hasa kwa somo la Hisabati.
Mkuu huyo wa
Shule aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Halmashauri ya
Wilaya ya Siha kwa kuwapatia mwalimu mmoja wa somo la
Biolojia na Jiografia katika ajira mpya zilizotolewa na Serikali hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha Valerian Juwal alieleza kuwa Wilaya ya Siha ilipata Walimu watatu wa masomo
ya Sayansi katika ajira mpya zilizotangazwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania hivi karibuni.
Alisema kuwa kati ya Walimu watatu wa masomo
ya Sayansi na Hisabati waliopangwa Wilaya ya Siha mwalimu mmoja alipangwa shule
ya Sekondar Fuka na wengine katika shule ya Sekondari Sanya Juu na shule ya
Sekondari Nuru.
Hata hivyo alieleza kuwa Serikali bado
itaendelea kuajiri Walimu wa masomo ya Sayansi kwa shule za Msingi na Sekondari
kwani mahitaji bado ni makubwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Siha aliwataka
Wananchi na wadau wa maendeleo kuendelea
kukamilisha ujenzi wa maabara kwani ndiyo suluhisho la pekee litakalosaidia
kupatikana kwa wataalam wa Sayansi na Hisabati.
Wilaya ya Siha inahitaji jumla ya Walimu 54 wa Masomo ya Sayansi na Hisabati kwa shule za Sekondari za Serikali.
No comments:
Post a Comment