Tuesday 16 May 2017

Siku za Wateka Bodaboda Zinahesabika Wilayani Siha

Mkuu wa Wilaya ya Siha  Mhe Onesmo Buswelu awaonya  wale wote wanaojihusisha na utekaji wa waendesha bodaboda  Wilayani Siha na kuchukua pikipiki zao kuwa siku zao zinahesabika.

Mkuu huyo wa Wilaya    ya Siha aliyasema hayo  katika mkutano wa Wananchi wa Kata ya Kirua pamoja na wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule ya Sekondari Fuka leo jumanne tarehe 16.5.2017. 

Alieleza kuwa hivi karibuni kuna tukio moja la kusikitisha lilitokea kwa bodaboda mmoja kutekwa katika Kijiji cha Sanya Juu na kisha kuuwawa na pikipiki yake kuchukuliwa na watu wanaosemekana kuwa ni  watekaji.

alisema Serikali ya Wilaya ya Siha imeshawakamata  watu watatu waliohusika na tukio hilo na wapo katika mikono ya sheria ili wachunguzwe na kisha wapatiwe  adhabu kulingana na makosa yao waliyotenda.

Aliwataka Wananchi na raia wema kuendelea kutoa taarifa za  matukio na maandalizi yote ya makundi ya kihalifu kwa Jeshi la Polisi ili hatua za Haraka zichukuliwa kwa Wahalifu kabla hawajatimiza malengo yao.

Aliwataka vijana kujishughulisha na shughuli halali za kujipatia kipato kwani Matendo ya kihalifu kwa Serikali ya Mhe Magufuli hayana nafasi tena na badala yake vijana watekeleze kaulimbiu ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania HAPA KAZI TU

No comments:

Post a Comment