Wakulima wa Wilaya ya Siha mkoa
wa Kilimanjaro wameweka mikakati ya kulirudisha katika ubora wake zao la kahawa
kama ilivyokuwa hapo miaka ya 1970 na mwaka 1960.
Mpango huo umewekwa na wakulima
wa zao la Kahawa Wilayani Siha leo tarehe 15.5.2017 katika ukumbi wa mikutano
wa Halmashauri ya Siha walipokutana na kufanya kikao cha pamoja na Mkuu wa
Wilaya ya Siha Mhe. Onesmo Buswelu.
Katika kikao hicho cha kazi
Wakulima hao walimweleza Mkuu wa Wilaya ya Siha changamoto mbalimbali
zilizosababisha kushuka kwa uzalishaji wa zao la Kahawa Wilayani Siha.Miongoni
mwa sababu hizo ni pamoja na:-
·
Kushuka kwa bei ya kahawa kutoka kwa wanunuzi
binafsi pamoja na vyama vya ushirika
·
Ukame wa muda mrefu katika Wilaya ya Siha
·
Kukosekana kwa mbegu bora ya zao la kahawa
·
Hali ya kukata tama kwa baadhi ya wakulima na
badala yake kutafuta zao mbadala
Akishiriki katika kikao
hicho,Mkuu wa Wilaya ya Siha aliwataka wakulima kutokata tamaa ya bei kwani
Serikali itasimamia kwa karibu kuhakikisha kuwa wakulima wanapata haki yao
kulingana na bei ya soko.
No comments:
Post a Comment