Sunday, 17 April 2016

SIHA YAPANDA MITI ZAIDI YA NUSU MILIONI



Halmashauri ya Wilaya ya Siha yapanda miti zaidi ya 540,000 hadi kufikia mwisho wa mwezi Machi 2016

Mkuu wa Idara ya ardhi na maliasili jonas P M kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji, alimueleza mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro wakati akisoma taarifa fupi ya upandaji miti Wilaya ya Siha iliyofanyika kimkoa tarehe 15.4.2016

Alieleza kuwa katika uzinduzi huo wa upandaji miti eneo la makao makuu ya halmashauri jumla ya miti 10300 itapandwa kwa kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa maendeleo vikiwemo Red Kros Tanzania na kikundi cha Wanamazingira Floresta
Taarifa hiyo pia ilieleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Siha inampango wa kuotesha miti zaidi ya 1.7 Mil kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji alimueleza mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro baadhi ya changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na wanyama pori na wanyama wa kufugwa pamoja na ukame wa mara kwa mara.

Aliemueleza mkuu wa mkoa kuwa wananchi wa Wilaya ya siha wamehamasika vya kutosha katika zoezi la kupanda miti na wenyewe wapo tayari kupanda miti katika maeneo yao bila hata kusimamiwa.

No comments:

Post a Comment