Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
Mh.Said Meck Sadiki ameagiza halmashauri zote Mkoa wa Kilimanjaro kuwa na
bustani za vitalu vya miti na kugawa miti hiyo bure kwa wananchi
Hayo ameyasema alipokuwa
katika maadhimisho ya siku ya upandaji miti kimkoa ambayo yalifanyika katika
Halmashauri ya Wilaya ya Siha tarehe 15.4.2016
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
alishiriki kwa kupanda miti zaidi ya 10,000 iliyopandwa katika eneo la makao
makuu ya Halmashauri ya siha, ambapo wananchi,watumishi na kikundi cha Floresta
Mkuu huyo wa mkoa alisema
kuwa sasa wakati umefika kwa kila halmashauri kutenga bajeti za kuendesha bustani
za vitalu vya miche ya miti itakayogawiwa bure kwa wananchi na taasisi zote za
serikali hasa shule za msingi na sekondari
‘’Kanzia sasa lazima kila
wilaya kuhakikisha kuwa inamiliki kitalu cha miche ya miti ambayo itasaidia
upatikanaji wa miti ya kupanda hasa wakati wa msimu wa mvua kama ilivyo hivi
sasa’’alisema mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
Hadi sasa Halmashauri ya
Wilaya ya siha inabustani ya miche ya miti ambayo inauwezo wa kuwa na miche
zaidi ya 1.5Mil kwa wakati mmoja
Aidha halmashauri ya Wilaya
ya Siha ilianzisha mpango wa kuwa na kitalu cha miche ya miti kinachomilikiwa
na Halmashauri kuanzia mwaka 2012 na miche inayozalishwa katika kitalu hicho
hugawanywa bure kwa wananchi,Taasisi za
Umma na ofisi za kata na vijiji
No comments:
Post a Comment