Wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro imeazimisha siku ya walemavu duniani kwa kuwa kuwakutanisha walemavu wa aina mbalimbali
maadhimisho hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa KKKT Jimbo la Siha kwa kuwakutanisha walemavu wa aina mbalimbali wakiwemo walemavu wa ngozi
katika maadhimisho hayo mkuu wa Wilaya ya Siha ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Dkt. Charles Mlingwa ndiye alikuwa mgeni wa heshima ambapo aliwataka wazazi wa Wilaya za Siha na Hai kuhakikisha kuwa wanawatendea vema kwa kuwalinda na kuwapa haki zao za msingi walemavu
hata hivyo Mlingwa kwa upande mwingine alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na madhehebu ya dini itaendelea kuwajali na kuwapa haki zinazostahili walemavu wote katika jamii
alieleza kuwa ipo changamoto kwa baadhi ya wazazi kuwaficha walemavu ndani na hivyo kufanya utambuzi wao kuwa mgumu hasa maeneo ya vijijini
Dkt Mlingwa aliendelea zaidi kusema kuwa hali hii ya kuficha walemavu ndani inatokana na baadhi ya mila na desturi za Makabila yetu ambayo wengine wanaamini kuwa kuwa na mtoto mlemavu ni laana katika familia
mimi kama mkuu wa Wilaya kwa niaba ya serikali sitakubali kuona jambo hilo linaendelea katika eneo langu la utawala hasa Wilaya hizi za Siha na Hai ambapo kwa sasa mimi ni mkuu wa Wilaya na mwakilishi wa Wananchi aliongeza Dkt Mlingwa
napenda kuagiza kwa msisitizo kuwa Serikali itafanya kila inaloweza kufanya kuhakikisha kuwa wale wote wanaowanyanyapaa na kuwanyanyasa walemavu wanachukuliwa hatua za kisheria mara moja
Naye kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha Abrahaman Kanji kwa upande wake alieleza kuwa Halmashauri ya Siha itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa walemavu wote hasa watoto wanapatiwa elimu stahiki bila ubaguzi wowote
aliipongeza KKKT jimbo la Siha kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuanzisha shule maalumu ya Msingi Faraja kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali.
aliwaomba Kanisa kwa kushirikiana na Serikali kuendelea na moyo huo wa kuwahudumia walemavua na hata wale wasiowalemavu na Halmashauri ya Siha itaendelea kushirikiana na Kanisa hilo
wilaya ya Siha inazoshule tatu za msingi na shule moja maalum kwa ajili ya utoaji wa elimu kwa watoto walio na ulemavu wa aina mbalimbali japokuwa shule hizo zinakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za miundombinu wa majengo
No comments:
Post a Comment