HALMASHAURI YA WILAYA
YA SIHA
TAARIFA KWA UMMA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha anapenda
kuwajulisha Wananchi wote wa Wilaya ya Siha kuwa maadhimisho ya kampeni ya
kupanda miti Kimkoa yatafanyika katika
Wilaya ya Siha tarehe 21/04/2016.
Katika maadhimisho hayo,Wananchi wanaombwa kujitokeza kwa
wingi katika eneo la makao makuu ya Halmashauri na katika maeneo mengine
watakayoelekezwa na viongozi wao kwa ajili ya kushirikiana zoezi la kupanda
miti. Mgeni rasmi katika maadhimisho
hayo atakuwa Mheshimiwa Said Meck Sadiki Mkuu wa
Mkoa wa Kilimanjaro. Aidha mh.mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro atashiriki zoezi la
kupanda miti na Wananchi eneo la makao makuu ya Halmashauri siku hiyo.
Wananchi wa maeneo Kata za jirani na Jengo la Makao Makuu ya
Halmashauri ya Wilaya ya Siha lililopo Kata ya Gararagua kwa jina maarufu Dutch Kona wanaombwa kufika kwa wingi
kwa ajili ya Kuunga mkono jitihada za Serikali za kutunza Mazingira
Katika maadhimisho hayo
zaidi ya miti 7,000 ya aina mbalimbali zitapandwa katika eneo la
kuzunguka makao makuu ya Halmashauri ya Siha.
Aidha, Maandalizi ya kupanda miti siku hiyo yamekamilika
ambapo Mkuu wa Wilaya ya Siha,Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Siha ni miongoni
mwa viongozi watakaoshiriki na Wananchi katika upandaji miti.
Katika kuitikia wito wa zoezi hilo leo wanavikundi mbalimbali
wa mazingira kutoka Wilaya ya Siha wamepanda miti zaidi ya 4,000 katika eneo
atakalopanda miti Mh Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro atakapojumuika na Wananchi
tarehe 21.4.2016
Katika mwaka wa fedha 2015/2016 Halmashauri ya Wilaya ya Siha
imeweka malengo ya kupanda miti zaidi ya 1.7 Mil katika maeneo mbalimbali
katika halmashauri hiyo
Limetolewa na
Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya (W) Siha
Tarehe 08/4/2016
No comments:
Post a Comment