Mkuu wa Mkoa wa
Kiliamanjaro Mh.Said Meck Sadiki amepiga marufuku matumizi ya misumeno ya
nyororo(chainsaw ) katika shughuli za mazao ya misitu bila kuwa na kibali maalum.
Mh Said Meck Sadiki alitoa
maagizo hayo alipokuwa katika maadhimisho ya siku ya upandaji miti mkoa Kilimanjaro
yaliyofanyika katika Wilaya ya Siha tarehe 15.4.206
Mkuu wa mkoa alisema kuwa
hali ya ukataji miti katika mkoa wa Kilimanjaro bado unaendelealicha ya katazo
la mkoa la kutaka miti isikatwe bila kibali maalum.
Mh mkuu wa mkoa alisema
kuwa ,mkoa umegundua kuwa matumizi ya chainsaw ndiyo sababu kubwa
inayosababisha uharibifu wa mazingira kwa kiasi kikubwa katika mkoa wangu.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
ameagiza kuwa watu wote wanaomiliki chainsaw kuzisalimisha kwa wakuu wa wilaya
na wakuu wa polisi wa wilaya kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria.
Aliwaambia wananchi kuwa
baada ya zoezi la kusalimisha chainsaw kukamilika mtu yeyote atakayekutwa na
chainsaw atahesabiwa kuwa ni mhalifu kama walivyo wahalifu wanaomiliki silaha
kinyume cha sheria.
Alibainisha kuwa ofisi yake
haitakuwa na mzaha na suala hili hasa ukizingatia umuhimu wa kutunza mlima
Kilimanjaro kwa manufaa ya wanakilimanjaro na Taifa kwa ujumla.
Alitoa wito kwa wananchi wa
Kilimanjaro kutoa ushirikiano wa kuwabainisha wale wote wanaomiliki chainsaw kinyume
na utaratibu mpya wa mkoa wa Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment