Wednesday 5 July 2017

Wananchi Wiri wajipanga kupambana na Uhalifu





Serikali ya Kijiji cha Wiri Kata ya Gararagua wameazimia kwa kauli moja kupambana na uhalifu wa aina yoyote katika kijiji hicho.

Maazimio hayo yamefanyika wakati viongozi wa Serikali ya kijiji cha Wiri walipokutana katika ofisi za Kijiji hicho hivi karibuni kwa lengo kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo ya wananchi huku agenda ya ulinzi na usalama ikitiliwa mkazo na wajumbe wengi.

Katika kikao hicho wajumbe walimshukuru Mhe. Onesmo Buswelu mkuu wa Wilaya ya Siha kwa agizo lake la kukataza usafirishaji,na biashara ya mahindi ya kuchoma kwani katazo hilo limesaidia kupunguza wizi na udokozi wa mahindi mabichi ambao ulikuwa umeanza kushika kasi siku za hivi karibuni.

Mwenyekiti wa kijiji cha Wiri mhe. Hamza Munisi alieleza kuwa Serikali yake imejipanga kuhakikisha kuwa matukio yote ya uhalifu yatakapotokea yanadhibitiwa mara moja.

Aidha,alieleza kuwa hadi sasa hali ya utulivu na amani katika kijiji chake ni salama kabisa na ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kushirikiana na viongozi wa serikali yake katika kuimarisha ulinzi na usalama pamoja suala zima la  maendeleo.




No comments:

Post a Comment