Sunday 15 May 2016

RATIBA YA MITIHANI YA MOCK KIDATO CHA NNE 2016 MKOA WA KILIMANJARO YATOLEWA RASMI

RATIBA YA MITIHANI YA MOCK MKOA WA KILIMANJARO KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE 2016 HII HAPA

tarehe                                              asubuhi (8;00-11:00                                               mchana

16.5.2016                                        B/MATHS(STEP)                                                 KISWAHILI
17.5.2016                                        B/MATHS                                                       KISWAHILI(STEP)
18.5.2016                                        BIOLOGY(STEP)                                          HISTORY
19.5.2016                                        BIOS PRACTICAL(STEP)                           ENGLISH(STEP)
20.5.2016                                        BIOS PRACTICAL 2(STEP)                        B/KEEPING
23.5.2016                                        E/LANGUAGE                                             GEOGRAPHY
24.5.2016                                        PHYSICS                                                      CIVICS
25.5.2016                                        BIOS                                                              LITERATURE
26.5.2016                                   F.NUTRITIONS                                                 COMMERCE
27.5,2016                                   ADD. MATHS                                                    AGRICULTURE
30.5.2016                                   MUSIC,PHYSICAL EDUC                                MECHANICS
31.5.2016                                     WORKSHOP                                  B/KNOWLEDGE,D/KIISKAM
01.6.2016                                    CHEMISTRY                              B/KNOWLEDGE 2,D/KIISLAM 2

                     
        


Wednesday 11 May 2016

KIDATO CHA SITA WAMALIZA MITIHANI YAO SHULE 4 ZA SIHA

Wanafunzi wa kidato cha sita katika shule za Sekondari wilayani Siha wahitimu mitihani ya kidato cha sita kwa mwaka 2016 katika shule Nne za Sekondari Wilayani hapa.

Ofisa Elimu Sekondari Abrahaman Kanji alizitaja shule hizo kuwa ni Shule ya Sekondari Sanya Juu(Sanya Day),Oshara,Visitation na Faraja Siha.

alieleza kuwa kwa ujumla mitihani imefanyika kwa kufuata utaratibu unaotakiwa na baraza la mitihani la Taifa kwa kuzingatia maelekezo ,taratibu na Sheria zote za Mitihani ya Taifa kufanyika.

Kati ya Shule hizo nne Mbili zinamilikiwa na  Serikali na nyingine na mashirika ya Dini. Wilaya ya Siha inajumla ya shule 6 za kidato cha tano na Sita  4 za Serikali na 2 za mashirika ya Dini zenye kuchukua wanafunzi katika michepuo ya masomo ya  Sayansi na Sanaa.

WANAFUNZI WAPATIWA CHANJO YA MINYOO SIHA

baadhi ya wanafunzi Wilayani Siha wakisubiri kupatiwa chanjo ya minyoo leo katika shule mbalimbali Wilayani humo. zoezi la chanjo limefanyika leo tar 11.5.2016 kwa watoto wenye umri kati ya miaka 4 hadi 14 wengi wao wakiwa wanafunzi wa shule za msingi

WATOTO ZAIDI YA 24000 KUPATIWA CHANJO YA MINYOO SIHA

Wilaya ya Siha inategemea kutoa chanjo ya minyoo kwa watoto zaidi ya 24000 kwa mwaka 2016.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Rashid Kitambulio  amewataka wananchi na wakazi wote wa Siha kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha zoezi hilo muhimu kwa maendeleo ya watoto wetu na Taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi amewataka wazazi kuhakikisha kuwa watoto wote wenye umri wa miaka 4 hadi 14 wanapatiwa chanjo hiyo muhimu kwa ajili ya minyoo. alieleza kuwa wataalam wa afya kwa kushirikiana na Walimu watahakikisha wanasimamia zoezi hilo kwa ukamilifu ili kutimiza malengo ya kuwachanya watoto wote katika Wilaya ya Siha.

alitoa wito kwa wazazi kushirikiana na watoa huduma ili kila mtoto anayestahili apatiwe chanjo kwa wakati. Aliongeza kuwa chanjo hiyo inatolewa bure bila malipo yoyote na kuwatoa hofu wazazi wanafikiri kuwa watatakiwa kufanya malipo.

Hata hivyo mkurugenzi wa Halmashauri ya Siha alieleza kuwa matayarisho ya vifaa vyote vinavyotakiwa vimekamilika na zoezi limeanza leo tarehe 11.05.2016 katika kata zote 17 zilizopo Wilayani Siha. Alisema kuwa zoezi hilo litaendelea tarehe 12 na 13 kama halitakamilika kwa siku moja lengo ni kuhakikisha kuwa walengwa wote wanapata huduma.



Tuesday 3 May 2016

MITI ZAIDI YA 1.7 MIL KUPANDWA SIHA MWAKA 2016

makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro

mkutano wa Baraza la Madiwani Tarehe 6.5.2016

TANGAZO

MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI KWA KIPINDI CHA ROBO YA TATU (JANUARI HADI MACHI ,2016) UTAFANYIKA TAREHE 6.5.2016 SAA 4:00 ASUBUHI.


MKUTANO HUO UTAFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA HALMASHAURI YA WILAYA YA  SIHA.


WOTE MNAKARIBISHWA

limetolewa na Kitengo cha habari na Mawasiliano (W) SIHA
tarehe 03 Machi,2016

VIKUNDI VYA MAZINGIRA SIHA VYAJITOLEA KUPANDA MITI ZAIDI YA 10,000

 baadhiya vikundi vya mazingira Wilaya ya Siha wakipanda miti eneo la makao makuu ya Halmashauri hivikaribuni





RC KILIMANJARO APONGEZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA MSITU WA WEST KILIMANJARO

 Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro Mh. Said Meck Sadiki akiwa ndani ya hifadhi ya mlimaKilimanjaro eneo la Londros gate Wilayani Siha na kukagua uhifadhi wa mazingira

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,uongozi wa Wilaya ya Siha na baadhi ya Wataalam wakiwa katika hifadhi ya Taifa ya MlimaKilimanjaro hivi karibuni katika shughuli za kukagua hifadhi hiyo

RC KILIMANJARO AKAGUA SHAMBA LA MITI WEST KILIMANJARO WILAYANI SIHA

 MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO MH.SAID MECK SADIKI AKIPEWA MAELEZO YA JINSI YA KUHAMISHA MICHE YA MITI KUTOKA KITALUNI NA KWENDA KATIKAVIRIBA.HAYO YALIFANYIKAKATIKA SHAMBA LA MITI WEST KILIMANJARO TARAFA YA SIHA MAGHARIBI


hii ni mojawapo ya bustani ya miti katika shamba la miti West Kilimanjaro iliyokaguliwa na Mkuuwa Mkoa wa Kilimanjaro mh. Said M Sadiki katika ziara fupi aliyoifanya hivi karibuni Wilayani Siha. Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kukagua shughuli za shamba hilona uhifadhi wa mazingira

SIKU YA UPANDAJI MITI MKOA WA KILIMANJARO YAFANYIKA WILAYANI SIHA 2016

 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Said Meck Sadiki akishiriki maadhimisho ya upandaji miti Mkoa wa Kilimanjaro yaliyofanyika Wilayani Siha tarehe 15.4.2016 eneola makao makuu ya Halmashauri ya Siha. zaidi ya miti 10,000 ilipandwa siku hiyokatika eneo hilo 

 Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Siha ambaye pia ni DMO wa Wilaya ya Siha Dr. Best Magoma akishiriki katika zoezi laupandaji miti Kimkoa  tarehe 15.4.2016
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Siha Mh.Frank Kisinane akishiriki katika zoezi laupandaji miti Kimkoa katika eneo la makao makuu ya Halmashauri hiyo tarehe 15.4.2016