Sunday 17 April 2016

CHAINSAW SASA MARUFUKU MKOA WA KILIMANJARO




Mkuu wa Mkoa wa Kiliamanjaro Mh.Said Meck Sadiki amepiga marufuku matumizi ya misumeno ya nyororo(chainsaw ) katika shughuli za mazao ya misitu bila kuwa na kibali maalum.

Mh Said Meck Sadiki alitoa maagizo hayo alipokuwa katika maadhimisho ya siku ya upandaji miti mkoa Kilimanjaro yaliyofanyika katika Wilaya ya Siha tarehe 15.4.206

Mkuu wa mkoa alisema kuwa hali ya ukataji miti katika mkoa wa Kilimanjaro bado unaendelealicha ya katazo la mkoa la kutaka miti isikatwe bila kibali maalum.

Mh mkuu wa mkoa alisema kuwa ,mkoa umegundua kuwa matumizi ya chainsaw ndiyo sababu kubwa inayosababisha uharibifu wa mazingira kwa kiasi kikubwa katika mkoa wangu.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ameagiza kuwa watu wote wanaomiliki chainsaw kuzisalimisha kwa wakuu wa wilaya na wakuu wa polisi wa wilaya kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria.

Aliwaambia wananchi kuwa baada ya zoezi la kusalimisha chainsaw kukamilika mtu yeyote atakayekutwa na chainsaw atahesabiwa kuwa ni mhalifu kama walivyo wahalifu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria.

Alibainisha kuwa ofisi yake haitakuwa na mzaha na suala hili hasa ukizingatia umuhimu wa kutunza mlima Kilimanjaro kwa manufaa ya wanakilimanjaro na Taifa kwa ujumla.

Alitoa wito kwa wananchi wa Kilimanjaro kutoa ushirikiano wa kuwabainisha wale wote wanaomiliki chainsaw kinyume na utaratibu mpya wa mkoa wa Kilimanjaro.

SIHA YAPANDA MITI ZAIDI YA NUSU MILIONI



Halmashauri ya Wilaya ya Siha yapanda miti zaidi ya 540,000 hadi kufikia mwisho wa mwezi Machi 2016

Mkuu wa Idara ya ardhi na maliasili jonas P M kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji, alimueleza mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro wakati akisoma taarifa fupi ya upandaji miti Wilaya ya Siha iliyofanyika kimkoa tarehe 15.4.2016

Alieleza kuwa katika uzinduzi huo wa upandaji miti eneo la makao makuu ya halmashauri jumla ya miti 10300 itapandwa kwa kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa maendeleo vikiwemo Red Kros Tanzania na kikundi cha Wanamazingira Floresta
Taarifa hiyo pia ilieleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Siha inampango wa kuotesha miti zaidi ya 1.7 Mil kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji alimueleza mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro baadhi ya changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na wanyama pori na wanyama wa kufugwa pamoja na ukame wa mara kwa mara.

Aliemueleza mkuu wa mkoa kuwa wananchi wa Wilaya ya siha wamehamasika vya kutosha katika zoezi la kupanda miti na wenyewe wapo tayari kupanda miti katika maeneo yao bila hata kusimamiwa.

HALMASHAURI ZOTE KILIMANJARO ZATAKIWA KUWA NA BUSTANI ZA MICHE YA MITI



Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh.Said Meck Sadiki ameagiza halmashauri zote Mkoa wa Kilimanjaro kuwa na bustani za vitalu vya miti na kugawa miti hiyo bure kwa wananchi
Hayo ameyasema alipokuwa katika maadhimisho ya siku ya upandaji miti kimkoa ambayo yalifanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha tarehe 15.4.2016
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro alishiriki kwa kupanda miti zaidi ya 10,000 iliyopandwa katika eneo la makao makuu ya Halmashauri ya siha, ambapo wananchi,watumishi na kikundi cha Floresta
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa sasa wakati umefika kwa kila halmashauri kutenga bajeti za kuendesha bustani za vitalu vya miche ya miti itakayogawiwa bure kwa wananchi na taasisi zote za serikali hasa shule za msingi na sekondari
‘’Kanzia sasa lazima kila wilaya kuhakikisha kuwa inamiliki kitalu cha miche ya miti ambayo itasaidia upatikanaji wa miti ya kupanda hasa wakati wa msimu wa mvua kama ilivyo hivi sasa’’alisema mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
Hadi sasa Halmashauri ya Wilaya ya siha inabustani ya miche ya miti ambayo inauwezo wa kuwa na miche zaidi ya 1.5Mil kwa wakati mmoja
Aidha halmashauri ya Wilaya ya Siha ilianzisha mpango wa kuwa na kitalu cha miche ya miti kinachomilikiwa na Halmashauri kuanzia mwaka 2012 na miche inayozalishwa katika kitalu hicho hugawanywa  bure kwa wananchi,Taasisi za Umma na ofisi za kata na vijiji  

Wednesday 13 April 2016

MAADHIMISHO YA UPANDAJI MITI KIMKOA WILAYA YA SIHA 2016

  

HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA       
                                              TAREHE 13.4.2016 
TANGAZO KUHUSU  UPANDAJI MITI 
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA ANAWATANGAZIA WANANCHI NA  WATUMISHI WOTE KUWA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO MH. SAID M. SADIKI ATASHIRIKI MAADHIMISHO YA UPANDAJI MITI KIMKOA YATAKAYOFANYIKA WILAYA YA SIHA SIKU YA IJUMAA TAREHE 15.4.2016. 

AIDHA, SHUGHULI HIYO ITAFANYIKA ENEO LA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA  SIHA KUANZIA SAA 3:00 ASUBUHI.


HIVYO WANANCHI NA WATUMISHI WOTE MNATAKIWA KUSHIRIKI VEMA KATIKA ZOEZI HILO MUHIMU LA UTUNZAJI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA.

LIMETOLEWA NA

Dkt. Best Magoma 
Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji Halmashauri  (W) SIHA 


Friday 8 April 2016

SIHA KUPANDA MITI ZAIDI YA 1.7 MIL






HALMASHAURI YA WILAYA YA SIHA
TAARIFA KWA UMMA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha anapenda kuwajulisha Wananchi wote wa Wilaya ya Siha kuwa maadhimisho ya kampeni ya kupanda miti Kimkoa yatafanyika  katika Wilaya ya Siha tarehe 21/04/2016.

Katika maadhimisho hayo,Wananchi wanaombwa kujitokeza kwa wingi katika eneo la makao makuu ya Halmashauri na katika maeneo mengine watakayoelekezwa na viongozi wao kwa ajili ya kushirikiana zoezi la kupanda miti. Mgeni rasmi  katika maadhimisho hayo atakuwa Mheshimiwa Said Meck Sadiki   Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Aidha mh.mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro atashiriki zoezi la kupanda miti na Wananchi eneo la makao makuu ya Halmashauri siku hiyo.

Wananchi wa maeneo Kata za jirani na Jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Siha lililopo Kata ya Gararagua kwa jina  maarufu Dutch Kona wanaombwa kufika kwa wingi kwa ajili ya Kuunga mkono jitihada za Serikali za kutunza Mazingira
Katika maadhimisho hayo  zaidi ya miti 7,000 ya aina mbalimbali zitapandwa katika eneo la kuzunguka makao makuu ya Halmashauri ya Siha.

Aidha, Maandalizi ya kupanda miti siku hiyo yamekamilika ambapo Mkuu wa Wilaya ya Siha,Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Siha ni miongoni mwa viongozi watakaoshiriki na Wananchi katika upandaji miti.

Katika kuitikia wito wa zoezi hilo leo wanavikundi mbalimbali wa mazingira kutoka Wilaya ya Siha wamepanda miti zaidi ya 4,000 katika eneo atakalopanda miti Mh Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro atakapojumuika na Wananchi tarehe 21.4.2016
Katika mwaka wa fedha 2015/2016 Halmashauri ya Wilaya ya Siha imeweka malengo ya kupanda miti zaidi ya 1.7 Mil katika maeneo mbalimbali katika halmashauri hiyo
Limetolewa na
 Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya (W) Siha
Tarehe 08/4/2016