Wednesday 7 August 2019

Madiwanni Siha wajifunza Kilimo & Ufugaji wa kisasa Nanenane Julai 6,2019

Madiwani wa Halmashauri ya Siha wakitembelea maonesho ya nanenane mwaka 2019 viwanja vya Njiro tarehe 6.8.2019 


 Mtaalam wa Chuo cha Nelson Mandela Arusha akielezea kuhusu matumizi sahihi ya madawa katika ukuzaji wa mazao ya chakula na biashara
 Elimu kuhusu matumizi ya maziwa kwa jamii imetolewa kwa Wah Madiwani wa Siha walipotembelea banda la Halmashauri ya Siha

 Bustani ya Siha imetia fora viwanja vya nanenane mwaka 2019
Wah. Madiwani wa Halmashauri ya Siha wakijifunza kuhusu kilimo bora ndani ya viwanja vya nanenane Arusha tarehe 6.8.2019

Friday 12 July 2019

Pata matokeo ya Kidato cha Sita shule za Sekondari Siha mwaka 2019


Bofya hapa kuona Matokeo ya shule za Siha
http://www.sihadc.go.tz/new/angalia-matokeo-kidato-cha-sita-2019-shule-za-siha

matukio ya Mwenge wa Uhhuru wapokelewa kwa Shangwe Wilayani Siha

 Wananchi wa Kata ya Ndumeti walivyoupokea Mwenge wa Uhuru ulipowasili Wilaya ya Siha mwaka 2019


Wananchi wa Kijiji cha Matadi Kata ya Ndumeti walivyopokea Mwenge wa Uhuru katika shule ya Sekondari matadi ulipowasili shuleni hapo tarehe 20.6.2019
Kata ya Ndumeti kijiji cha Matadi  ilivyotia fora katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2019  









Madiwani Siha wapanga mkakati wa kuimarisha mapato ya ndani ya Halmashauri


Baraza la Madiwani Halmashauri ya Siha wakisikiliza Mawasilisho  ya miradi mkakati inayotarajiwa kutekelezwa katika Halmashauri ya Siha -Kilimanjaro

 Mkuu wa Wilaya ya Siha mhe. Onesmo Buswelu akiongea na Waheshimiwa Madiwani walipokuwa katika mkutano wa kawaida wa baraza tarehe 11.7.2019
Waheshimu Madiwani wa Halmashauri ya Siha wakiwa katika mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani Siha tarehe 11.7.2019 

Mkuu wa Wilaya ya Siha mhe.Onesmo Buswelu akisema jambo katika Baraza la Madiwani Halmashauri ya Siha tarehe 11.7.2019

ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Wilaya ya Siha tarehe.7.7.2019

 Mkuu wa Wilaya ya Siha mhe Onesmo Buswelu akimpokea Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Siha tarehe 7.7.2019
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Siha mhe. Godson Ngomuo akimpokea katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa 

 Katibu Tawala wa Wilaya ya Siha Joseph Mabiti akisalimiana na katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa 

 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa ndugu Bashiru Ally akisalimiana na Wakuu wa Idara na Vitengo alipowasili katika Hospitali ya Wilaya ya Siha

 Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Siha Dkt. Barnabas Mbwambo akisalimiana na Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa
 Mbunge wa Jimbo la Siha Mhe. Godwin Mollel (katikati ) akipokea burudani kutoka ngoma za kabila la Kimaasai walipompokea katibu mkuu wa CCM Taifa
Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Bashiru Ally akifurahia ngoma ya kimaasai alipowasili katika Hospital ya Wilaya ya Siha

Monday 13 May 2019

WATUMISHI WANAMICHEZO SIHA WAFANYA ZIARA HIFADHI YA NGORONGORO



Timu ya mpira wa miguu ya watumishi wa Umma ikijiandaa na mchezo wa Bonanza
tarehe 4/5/2019 kati ya timu himu na Serena Hotel Timu

 Wachezaji wa Siha wakipeana mbinu za mchezo wakati wa mapumziko
Kikosi kamili cha watumishi wa Siha kilichosafiri kwenda kwenye Bonanza la michezo hifadhi ya Ngorongoro kuanzia tarehe 3/5/2019 hadi tarehe 5/5/2019
Mazoezi kabla ya mchezo ndiyo njia bora ya kuweka miili katika hali bora zaidi,timu ya Siha hapo juu ikijifua kabla ya mchezo wa Bonanza

Thursday 25 April 2019

BARABARA ZA SIHA ZABORESHWA

Wakala wa usimamizi wa barabara za mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Siha wameendelea kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya tano kwa vitendo kwa kuzifanyia matengenezo barabara za vijijini katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Siha.
Kwa Ujumla barabara zote katika Vijiji na Vitongoji Wilayani Siha zinapitika wakati wote na kusaidia shughuli mbalimbali za wananchi katika kusafiri na kusafirisha mazao mbalimbali ya biashara na chakula

Hii ni barabara ya Siha Sango hadi Kijiji cha Mese Wilayani Siha ikiendelea kufanyiwa matengenezo makubwa  kupitia TARURA

WAZAZI WATAKIWA KUWAPA ELIMU WATOTO BILA UBAGUZI-SIHA

Wananchi wa Wilaya ya Siha wameshauriwa kuwapa watoto wote elimu bila ubaguzi wa aina yoyote
Hayo yamesemwa na Mwalimu Rose Sandi  Afisa elimu shule za Msingi katika Halmashauri ya Wilayani  ya Siha  leo tarehe 2.04.2019 aliposhiriki na watoto wenye mahitaji maalumu (siku ya Usonji) katika maazimisho ya siku yao duniani.
Watoto wenye usonji wakishirikiana na wazazi wao katika zoezi la kupanda miti mapema leo katika shule ya msingi Sanya Juu
Maazimisho hayo katika Wilaya ya Siha yamefanyika katika shule ya Msingi Sanya juu na kujumuisha watoto wenye mahitaji maalumu kutoka shule mbalimbali za msingi Wilayani Siha ikiwemo shule ya Msingi  Faraja Siha .
Wanafunzi wa shule ya msingi Sanya Juu wakishiriki maazimisho ya siku ya Usonji dunia leo tarehe 2.4.2019
Katika Maazimisho hayo wazazi na jamii imetakiwa kuwapa elimu watoto wote katika familia bila   ubaguzi wa jinsia,maumbile au uwezo wa watoto katika kuelewa na kuchanganua mambo mbalimbali.

SIHA YAPATA MAFANIKIO UTOAJI ELIMU MAALUM

SIHA YAPATA MAFANIKIO ELIMU MAALUM
Halmashauri ya Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro imekuwa miongoni mwa Halmashauri za mfano katika kutoa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalumu (watoto wenye Usonji).Hayo yamebainika katika maazimisho ya siku ya Usonji dunia ambayo kila mwaka hufanyika tarehe 2 April,,ambapo katika Wilaya ya Siha mwaka 2019 yamefanyika katika Shule ya Msingi Sanya Juu.
Katika kutekeleza uboreshaji wa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum,Halmashauri ya Wilaya ya Siha inazo jumla ya shule 4 za msingi zinazotoa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum(Usonji) ,shule hizo ni pamoja na Shule ya Msingi Nuru,Sanya Juu,Faraja na shule ya Msingi Naibili.
Katika shule hizo kwa mwaka huu 2019 zina jumla ya watoto 147 ambapo watoto wote wanaosoma wana mahitaji maalum(Usonji) ,Aidha walimu wenye taaluma ya kutosha na waliobobea wanafundisha shule hizo kulingana na mahitaji ya watoto husika.
Kuwepo kwa mafanikio haya kumetokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya wazazi na wadau mbalimbali wa elimu ikiwemo Serikali ya awamu ya tano ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo mdau namba moja katika kufanikisha zoezi hili muhimu la kuwapatia elimu watoto wa Kitanzania bila kujali tofauti za kijinsia,maumbile wala maeneo mtoto anapotoka.
Katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano (2015 hadi sasa 2019) tumeshuhudia ongezeko kubwa la wanafunzi wenye mahitaji maalum wakipelekwa mashuleni na wazazi pamoja na walezi wao, hii imetokana na Sera nzuri ya Serikali ya awamu ya Tano ya utoaji wa elimu bila malipo katika shule zote za Serikali kuanzia ngazi ya awali hadi elimu ya kidato cha nne.
Watoto wenye mahitaji maalum wakishiriki zoezi la upandaji wa Miti katika eneo la shule ya Msingi Sanya Juu tarehe 2.4.2019

Watoto wa  darasa la Nne na Tatu katika shule ya Msingi Sanya Juu wakifurahia kushiriki katika maazimisho ya siku ya Usonji Duniani tarehe 2.4.2019,ambapo Kiwilaya yalifanyika shule ya Msingi Sanya Juu.

Kupata ushauri uliotolewa kwa wazazi katika maazimisho hayo bofya 
1. Hapa

KINAPA WATOE MSAADA AJALI YA MOTO VISITATION GIRLS -SIHA

Mamlaka ya hifadhi ya mlima Kilimanjaro (KINAPA) leo tarehe 5.4.2019 wametoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana Visitation kutokana na janga la moto lililotokea hivi karibuni na kuunguza vifaa mbalimbali vya wanafunzi wa shule hiyo.
Akiwasilisha msaada huo kwa Mkuu wa shule hiyo,Mwakilishi wa hifadhi ya Taifa ya mlima Kilimanjaro KINAPA ndugu Elibariki Eliangilisa alieleza kuwa KINAPA wametoa vifaa mbalimbali kwa wanafunzi wa shule hiyo  vyenye thamani ya shilingi milioni 2 ikiwa ni sehemu ya mchango wao kama wadau wakubwa wa elimu na lengo likiwa ni  kuwapa pole wanafunzi waliopoteza vifaa vyao wakati wa janga la moto.
Alieleza kuwa msaada walioutoa ni juhudi za Mhe. Onesmo Buswelu Mkuu wa Wilaya ya Siha ambaye aliwashirikisha kuhusu tukio la wanafunzi wa shule ya Wasichana Visitation kupoteza vifaa vyao mara baada ya tukio la moto kutokea katika bweni moja la wanafunzi,ambapo taarifa zinasemekana kuwa huenda ilitokana na hitilafu ya umeme,tunashukuru Mungu kuwa katika tukio hilo hakana madhara yoyote ya mwanafunzi kupata madhara bali ni vifaa tu ndio vilivyoteketea kwa moto.
“Naomba mpokee msaada wetu mdogo kwenu uwe kama chachu ya kuendelea kudumisha mahusiano yetu kama wahifadhi wa mlima na jamii ya watu wa Kilimanjaro” alisema Elibariki
Miongoni mwa vifaa vilivyokabidhiwa kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Visitation na Mwakilishi wa KINAPA kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ni pamoja na mashuka 100,Madaftari 150,Kalamu boksi 10, pamoja na vifaa vingine vingi vitakavyowezesha wanafunzi kujikimu


Wanafunzi wa shule ya wasichana Visitation  leo tarehe 5.4.2019 wakipokea msaada wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na mamlaka ya hifadhi ya mlima Kilimanjaro (KINAPA)
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Visitation wakishiriki katika kupokea vifaa mbalimbali vya msaada vilivyotolewa na mamlaka ya hifadhi ya Taifa ya mlima Kilimanjaro
wanafunzi wa shule ya wasichana Visitation wakishuhudia vifaa mbalimbali vya msaada vilikabidhiwa shuleni hapo na mwakilishi wa KINAPA

Vifaa mbalimbali vya msaada  vilivyotolewa na hifadhi ya Taifa ya mlima Kilimanjaro vikishushwa katika gari ,huku wanafunzi wa shule ya Visitation wakifurahia