Thursday 6 July 2017

Vikundi 12 vya wanawake wajasiriamali Siha wapatiwa elimu ya uendeshaji wa vikundi na matumizi ya mikopo

 Viongozi wa vikundi 12 vya wanawake wajasiriamali Wilaya ya Siha wakishiriki katika mafunzo ya ujasiriamali yanayoendelea leo tarehe 06.07.2017 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Siha.mafunzo hayo yameandaliwa na Halmashauri ya siha kwa lengo la kuwajengea uwezo wanawake wajasiriamali Wilaya ya siha.
Afisa maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Siha ndugu Ludovick Mushi akitoa mafunzo kwa viongozi wa vikundi vya wanawake wajasiriamali Wilaya ya Siha.mafunzo hayo yamefanyika leo tarehe 06.07.2017 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya siha mkoa wa kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment