Tuesday 11 July 2017

RC Kilimanjaro ajitambulisha kwa watumishi wa Umma Siha


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro mhe Anna Mghwira afanya ziara ya siku moja katika Wilaya ya Siha na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ziara hiyo imefanyika tarehe 10.07.2017 ambapo Mhe Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro amepata fursa ya kujitambulisha kwa watumishi wa serikali waliopo ofisi ya mkuu wa wilaya pamoja na wale wa halmashauri ya Siha.

Aidha mkuu huyo wa mkoa amepata nafasi ya kutembelea miradi ya maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Sanya Juu Elerai kwa kiwango cha lami kilomita 32.2  inayogharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania.

Pia mkuu wa mkoa alipata nafasi ya kutembelea hospital ya Wilaya ya Siha na kujionea shughuli za ujenzi zinazoendelea katika hospital hiyo zikiwemo za wodi ya wazazi inayogharamiwa na nguvu za wananchi na wadau wa maendeleo pamoja na ukamilishwaji wa jengo litakalotumika kwa ajili ya chumba cha upasuaji na kulaza wagonjwa ambapo  serikali imetoa shilingi milioni 250.

katika ziara hiyo ,pia mkuu wa mkoa alitembelea shamba la Kifufu na kujionea jinsi mwekezaji anavyofanya kazi ya kutekeleza agizo la serikali ya awamo ya tano la uchumi wa viwanda,ambapo mwekezaji amefanikiwa kuwa na machine za kusafisha mapararachichi tayari kwa kusafirisha nje ya nchi.

Mkuu wa Mkoa aliipongeza wilaya ya Siha kwa jitihada kubwa za maendeleo inazoonyesha hasa ukizingatia kuwa wilaya ya Siha bado ni changa na pamoja na kuwa na vyanzo vichache vya mapato ya ndani.

 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mhe Anna Mghwira akikaribishwa na watumishi wa Umma na viongozi wa halmashauri  katika Makao makuu ya halmashauri ya Siha katika ziara yake tarehe 10 .07.2017 wilaya ya Siha

No comments:

Post a Comment