Tuesday 11 July 2017

RC Kilimanjaro atoa somo kwa Watumishi wa Umma Siha


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira amewataka watumishi wa Umma katika wilaya ya Siha kufanya kazi kwa kuzingatia uzalendo,utu na uadilifu ili kutimiza malengo ya Serikali ya Tanzania.

Hayo ameyasema katika ziara ya siku moja iliyofanyika wilaya ya Siha  tarehe 10.07.2017  alipokutana na watumishi wa Serikali katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Siha.

Mkuu wa mkoa aliwataka watumishi wa Umma  Wilayani Siha kuendelea kuchapa  kazi kwa bidii na maarifa kwa kujiwekea malengo ya kazi ili iwe rahisi kwa kila mtumishi kujifanyia tathmini ya kazi anayofanya kila siku wawapo ofisini.
Alitoa wito kwa watumishi wote wa umma kujiepusha na mambo ya rushwa sehemu ya kazi kwani rushwa huondoa haki kwa watu wanaostahili kuipata hasa wananchi wa kipato cha chini.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira alikutana na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha tarehe 10.07.2017 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Siha


  Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro mhe Anna Mghwira(aliyevaa kitambaa) akipokelewa na viongozi wa halmashauri ya Siha katika ziara yake ya siku moja wilayani Siha tarehe 10 Julai,2017

No comments:

Post a Comment