Tuesday 4 July 2017

Siha kupata zaidi ya tani elfu 30 za Mahindi msimu wa mwaka 2017





Wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro inatarajia  kupata zaidi ya tani elfu 30 za mahindi msimu wa mavuno 2017 unaotarajiwa kuanza hivi karibuni. 

Kwa mujibu wa tathmini iliyofannya  mwezi Mei,2017 na wataalam wa Kilimo katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Wilaya ya Siha inatarajia kupata mavuno ya mahindi jumla ya tani 30,510 kwa msimu huu wa masika mwaka 2017. 

Aidha Wilaya  ya Siha inatarajia kuvuna tani 29,145 za mazao mengineyo yakiwemo maharage,viazi mviringo,karoti,njengere,mbaazi na mazao mengine yakiwemo ya mbogamboga  katika msimu wa masika mwaka 2017 na kufanya matarajio ya uzalishaji wa mazao kwa mwaka 2017 kufikia jumla ya tani 59,655.22.

Aidha,kutokana na matarajio ya uzalishaji Wilaya ya Siha inatarajia kuwa na ziada ya chakula tani 2,915 zinazotokana na uzalishaji wa mahindi, Mahitaji ya chakula (mahindi) Wilayani Siha kwa mwaka ni tani 27,595 tu .

Kwa mujibu wa sense ya watu na makazi ya mwaka 2012 Wilaya ya Siha inajumla ya watu 16313 wanawake wakiwa 59813 na wanaume wakiwa 56500

No comments:

Post a Comment